Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
NDOTO
kubwa ya wanandinga wa Tanzania na Afrika nzima ni kucheza soka la
kulipwa katika ligi kubwa duniani kama vile ligi kuu nchini England,
Hispania, Ujerumani, Ufaransa, na Italia.
Hakuna
mwanasoka mwenye malengo asiwaze kucheza katika ligi hizo zilizosheheni
klabu zenye mvuto mkubwa zaidi duniani na wanasoka bora wa Dunia.
Hakika
ni sifa kubwa sana kwa mchezaji wa Kiafrika kuonekana katika runinga
akisakata kabumbu anga za kimataifa. Simaanishi anaishia kupata sifa tu,
bali hata `mkwanja` unaopatikana katika soka hilo ni mkubwa.
Nani asiyefahamu utajiri wa Samuel Eto`o, Didier Drogba, Yaya Toure na wengine wengi kutoka nchi za magharibi mwa Afrika.
Hapa
Tanzania bado hatujafanikiwa kupata wanasoka mahiri wa kwenda kucheza
ligi za wenzetu zaidi ya kuwaona wachezaji wetu wakienda kucheza ligi za
kawaida kabisa huko Uarabuni na mataifa ya kiwango cha chini kisoka
barani Ulaya.
Wengine
kama Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu wamejaribu na
wamethubutu na ndio maana unawasikia na kuwaona TP Mazembe ya Jamhuri ya
kidemokrasia ya Kongo.
TP
Mazembe ni moja ya klabu kubwa yenye utajiri mkubwa barani Afrika. Kwa
wachezaji wa Kitanzania ni moja ya klabu inayowafaa na ndio maana
Samatta alitajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaowania tuzo ya
mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani.
Kocha Kaijage akiwa na vijana wake kwenye moja ya mazoezi ya Twiga Stars uwanja wa Karume, jijini Dar es salaam
Ukiwauliza
wachezaji wengi wa Tanzania, nini malengo yao? Jibu huwa ni jepesi sana
“nataka kucheza soka la kulipwa”. Sio tatizo kwa jibu hili, lakini bado
ipo haja ya kujiuliza tena, huyu anayetaka kucheza soka hilo anaweza
kutimiza ndoto hizo?.
Swali
hili huwa linanikosesha majibu ya haraka kila nikitafakari hali halisi
ya wachezaji wa Kitanzania ambapo wengi wao wana malengo makubwa, lakini
utekelezaji wake ni mdogo sana, nidhamu mbovu na kulewa sifa wakati
bado hajafanikiwa malengo yake.
Achana na hayo, kwasasa Dunia inajadili sana soka la wanawake.
No comments:
Post a Comment