Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya CXC ya jijini Dar es Salaam, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF) na waandaaji wa Tamasha la Pasaka wamejitosa kupiga tafu Mkutano
Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA)
utakaofanyika kesho.
Akizungumza
Dar es Salaam , Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando, alisema NSSF
imetoa udhamini wa ukumbi wakati CXC na Tamasha la Pasaka kila mmoja
ametoa Sh milioni moja kwa ajili ya mkutano huo utakaoenda pamoja na
Uchaguzi Mkuu wa chama hicho.
“Tunashukuru
Kampuni ya CXC ya jijini Dar es Salaam, waandaaji wa Tamasha la Pasaka
kampuni ya Msama Promotions na shirika la NSSF wametusaidia kwa kiasi
fulani mkutano wetu.
“Bajeti
yetu ni kubwa sana ni zaidi ya Sh milioni 10 maana licha ya wanachama
wa Dar es Salaam pia tuna wanachama kutoka mikoani, ambapo wengine
wanatoka Morogoro, Tanga, Zanzibar na Arusha,” alisema Mhando na
kuongeza kuwa wanatarajia wanachama 150 washiriki mkutano huo.
Alisema
mkutano utafanyika ukumbi wa NSSF Waterfront Dar es Salaam na kwamba
wanachama kutoka nje ya Dar es Salaam wanatarajia kuwasili leo tayari
kwa mkutano huo wa aina yake.
No comments:
Post a Comment