Baadhi
ya Wafanyakazi Wanawake wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
(HESLB) wakishusha mahitaji kutoka kwenye gari tayari kuikabidhi wa
uongozi wa ORCI. Baadhi
ya Wafanyakazi Wanawake wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
(HESLB) wakijiandaa kuingia katika wodi la kwanza la wanaume ambako kuna
wagonjwa 60.
……………………………………………………………………………….
WAFANYAKAZI
Wanawake wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
wameadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kutoa misaada kwa wagonjwa
takriban 200 waliolazwa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) ya
jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya wafanyakazi wa wanawake wa HESLB ndani yaChama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Utafiti na
kazi nyinginezo (RAAWU), Bi Octavia Selemani amesema kuwa wameafikiana kufanya hivyo kama taasisi ili kutoa mchango wao kwa wanajamii ambao wanahitaji zaidi msaada na faraja kutokana na kuwa katika hali ya maradhi sugu ya saratani.
kazi nyinginezo (RAAWU), Bi Octavia Selemani amesema kuwa wameafikiana kufanya hivyo kama taasisi ili kutoa mchango wao kwa wanajamii ambao wanahitaji zaidi msaada na faraja kutokana na kuwa katika hali ya maradhi sugu ya saratani.
Katika
kutekeleza tukio hilo ambalo limefanyika wiki moja kabla ya kilele cha
Siku ya Wanawake Duniani, Wafanyakazi hao kutoka idara na vitengo
mbalimbali vya taasisi hiyo ya serikali, wametoa msaada wa bidhaa za
mahitaji ya kila siku ikiwa ni pamoja na mchele, unga wa sembe,
maharage, sukari, mafuta ya kupikia, sabuni za mche, sabuni za unga na
dawa za meno.
Msaada
huo wa thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2 ulikabidhiwa Jumamosi ya
Machi mosi, 2014 kwa Muuguzi Mkuu wa zamu Bi Ofarasia Muhoha (Registered
Nurse) kwa niaba ya uongozi wa taasisi hiyo.
Kuhusu
maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Machi 8, 2014, Bi Octavia
amesema kuwa siku hiyo wafanyakazi wanawake watashiriki shughuli za
maadhimisho ikiwa ni pamoja na kuandamana na kusikiliza hotuba ya mgeni
rasmi kupata ujumbe wa siku hiyo.
Baada
ya maandamano, watakaa pamoja, kuzungumza na kutathmini mchango wao wa
utendaji kazi katika kujenga taifa kwa kupima mafanikio dhidi ya
changamoto wanazokabiliana nazo na kutafuta mbinu za kupata mafanikio
zaidi.
Siku
ya Wanawake Duniani huadhimishwa Machi 8 kila mwaka ikiwa ni kumbukumbu
ya jitihada za wanawake katika masuala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii
kwa miaka iliyopita na kupanga mikakati ya mafanikio zaidi kwa miaka
ijayo.
Katika
baadhi ya nchi kama China, Russia, Vietnam na Bulgaria, siku hii ni ya
mapumziko na inaadhimishwa kwa wananchi kuonyesha jinsi wanavyothamini
na kutambua mchango wa wanawake katika maendeleo ya nchi zao.
Mwaka huu maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kitaifa yanafanyika kwa ngazi ya mkoa yakiongozwa na kauli mbiu isemayo, “Chochea Mabadiliko kuleta Usawa wa Kijinsia”, ikisisitiza
na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuzingatia masuala ya jinsia
katika kuandaa mipango, bajeti na programu za maendeleo katika jamii.
No comments:
Post a Comment