Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Ruvu Shooting
iliyochezwa jana (Machi 2 mwaka huu) imeingiza sh. 20,610,000 ambapo
kila klabu ilipata mgawo wa sh. 4,402,492 wakati Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 3,143,898.31.
Ni
ukweli usiofichika kuwa mashabiki wa Simba sc hawana imani tena na
kikosi chao chini ya kocha wao, Raia wa Croatia, Dravko Logarusic
kufuatia kukumbwa na matokeo mabaya mzunguko huu wa pili.
Katika mechi sita ilizocheza mzunguko huu wa pili, Simba imefungwa mechi mbili, kutoka sare mbili na kushinda mbili.
Ilishinda
mabao 4-0 dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora, uwanja wa Taifa, Ikatoka
sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar, uwanja wa Jamhuri, ikafungwa 1-0 na Mgambo
JKT Dimba la CCM Mkwakwani Tanga, ikasafiri mpaka Mbeya na kutoka sare
ya 1-1 na Mbeya City.
Baada
ya Mbeya ikarejea Dar es salaam uwanja wa Taifa na kufungwa mabao 3-2
na JKT Ruvu, hatimaye jana ikafanikiwa kupata ushindi wa pili dhidi ya
Ruvu Shooting baada ya kuilaza mabao 3-2, huku mshambuliaji wake hatari,
Amiss Tambwe akifikisha mabao 19 baada ya kufunga mawili jana kipindi
cha kwanza.
Simba na Yanga ni klabu kongwe hapa nchini na zimejizolea mashabiki lukuki kila kona ya Tanzania na nje ya Tanzania.
Imekuwa
ni suala la kawaida kwa timu hizi zinaposhuka dimbani, mashabiki wake
kufurika kwa wingi kuona namna vikosi vyao vinavyosakata kabumbu.
Mapato
ya mlangoni yamekuwa muhimu sana kuendesha klabu za Simba, Yanga
kutokana na kuwa na mtaji wa mashabiki wengi zaidi ya klabu yoyote
nchini.
No comments:
Post a Comment