Katibu
wa Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Shy-Rose
Bhanji (pichani) amerejea nchini baada ya ziara ya siku 10 ya Wabunge wa
EALA nchini Kenya na hicho ndicho alichokisema kwa Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Nimerejea
nchini baada ya ziara ya siku 10 nchini Kenya. Ziara hii ya wabunge wa
EALA ilikuwa kwa mwaliko wa Serikali ya Kenya lengo likiwa kuhamasisha
wananchi wa Kenya kupata ufahamu mkubwa juu ya Mtangamano wa Jumuiya na
faida zake. Tulipata nafasi ya kuonana na wananchi, wafanyabiashara,
wabunge, maseneta, magavana, asasi za kiraia na makundi mengine.
Ziara
hii imenifungua macho zaidi kwamba bado tuna kazi kubwa mbele yetu
kuhakikisha kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki inakuwa ni ya Wananchi
(people Centred Integration).
Kama
nilivojionea mwenyewe kwa upande wa maeneo mbalimbali tuliyoyafikia
bado mwamko wa ufahamu wa masuala ya EAC mdogo sana na kiu wa kuifahamu
ni kubwa.
Hata
hivyo Serikali ya Kenya kwa kuhakikisha wananchi wengi zaidi
wanashiriki kikamilifu juu ya masuala ya Jumuiya imefufua mpango huu wa
wabunge wa EALA kufika Kenya kuendelea na zoezi la uhamasishaji.
Ni
imani yangu kwamba na Serikali ya Tanzania itaiga mfano huu mzuri wa
kuwaalika wabunge wa EALA kufika nchini ili kuwafikia makundi mbalimbali
hapa nchini kwa lengo la kuhamasisha. Hata kwa upande wa Tz bado
ufahamu wa wananchi wengi zaidi juu ya masuala ya Integration ni
changamoto kubwa.
Lengo
kuu la uanzishwaji wa EAC ni kuinua hali ya kiuchumi kwa wananchi wa EA
ambao sasa ni takriban millioni 140. Na iwapo mwamko wa wananchi ni
mdogo basi lengo hili litachukua muda mrefu sana kufikiwa au
kutokufikiwa kabisa.
No comments:
Post a Comment