Ni
siku 100 tu, ni vigumu kuamini kuwa iko karibu. Inaonekana kama jana tu
kwamba Brazil imethibitishwa kuwa muandaaji wa FIFA World Cup 2014.
Nakumbuka msisimko niliohisi na kuona kuwa nchi yangu inaenda kwenye
hatua muhimu ya mpira katika Dunia hii.
Hata ingawa mimi sitakuwa uwanjani, lakini nimeanza kupata vipepeo
tumboni kama ambavyo nilikuwa nikikaribia mechi kubwa. Baada ya yote
kumalizika FIFA World Cup, itakuwa ni ya aina ya mwisho kwa Brazil,
tofauti na kujitangaza yenyewe kimataifa. Uangalizi utakuwa juu yetu na
ni nafasi kubwa kwetu kwa kuionyesha Dunia umuhimu kuhusu Brazil na watu
wa Kibrazil walivyo.
Wakati wa Kombe la Dunia la Olimpiki 2016 itakayofanyika Brazil,
tutakuwa na nafasi ya kuionyesha Dunia jinsi tunavyo penda michezo na
vilevile tulivyo na nguvu katika uchumi wetu. Brazil ni kiongozi mkubwa
Duniani kiteknolojia na kiongozi mkubwa wa uzalishaji wa Nyama, madini
na mzalishaji mkubwa wa soya duniani. Ni karibu sasa maelfu ya watalii
na waandishi wa kigeni watafika kwenye mlango wetu ulio wazi kujionea na
kugundua uhalisia wa Wabrazili.
Ingawa Brazili ni nchi kubwa kijamii, lakini tumefanya mambo mengi ya
kukabiliana na matatizo katika miaka ya hivi karibuni. Tuna utaifa
tofauti lakini tuna umoja mzuri kijamii na kimaendeleo katika ubunifu wa
juu. Ni nchi iliyojaliwa watu wenye uwezo mkubwa kiakili na inawatu
wengi wenye vipaji vikubwa katika michezo kama Neymar anavyocheza na
maajabu yake ya kuchezea mpira . Vilevile mziki wa Tom Jobim na sayansi
aliyoipata kutoka kwa Miguel Nicolelis, kama utafiti waliofanya na
kupata matumaini kuwa siku moja mifupa ya binadamu inaweza kutembea
tena.
Brazili ni nchi nzuri sana, na ni nchi iliyobarikiwa kuwa na hali ya
asili nzuri. Watalii wote watakaofika Brazil wakati wa Kombe la Dunia
wajiandae kukutana na hali ambayo hawataisahau na hawajawahi kuiona.
Vilevile watafurahia kutembelea fukwe za kusini na kujionea misitu na
mto wa Amazon, milima katika mji wa Rio de Janeiro ambayo ni sehemu
muhimu sana kwa watalii. Naamini kila mtalii ataondoka Brazil akiwa na
kumbukumbu nzuri katika maisha yake yote.
Brazili ni nchi nzuri na ya furaha sana. Tunawakaribisha watalii wote
katika Kombe la Dunia kwa mikono yote miwili na hadi tutakapo anza
kufanya kazi.
Kwa mwaka 2014 FIFA World Cup taasisi za mitaa na uongozi wa bodi ya
wanachama, nimeridhika mwenyewe kwa kuona uwezo wao na uzoefu walionao
wa kusimamia tamasha kubwa hili. Ndani ya miji yote 12 itakayofanyika
mashindano haya, nimeshuhudia maelfu ya watu wakihakikisha kuwa
mashindano ya Kombe la Dunia yanafanyika katika hali nzuri.
Tumekumbana na vikwazo vigumu katika maandalizi ya Kombe la Shirikisho
la FIFA mwaka jana ambapo tulikuwa wenyeji. Hayo siyo maoni yangu tu
bali maoni ya washabiki wote wanahabari, na vilevile Raisi wa FIFA
Joseph S. Blatter.
Chini ya miezi sita baadae kwa mafanikio tuliandaa tukio la changamoto
nyingine. Droo ya mwisho katika mji wa Costa do Sauipe Bahia. Na
tulipogundua ni katika miji ipi michezo itakapochezewa timu za mataifa
32 ambazo zitapinga mashindano zilijadiliana mipango yao ya
kiutekelezaji na uanachama wa LOC, FIFA na serikali ya Brazil.
Kubadilishana huku kwa mawazo na maoni baina ya waandaaji wa timu za
taifa ni mchakato unaoendelea, na tukio jingine muhimu la warsha ya timu
za taifa mjini Costao do Santinho katika mji wa Florianopolis
uliofanyika mwezi uliopita. Mada zikiwa kama vile , usalama, usafiri na
jinsi timu zitakavyohudumiwa vilijadiliwa kwa undani.
Hivi sasa tuko nyumbani moja kwa moja , toka mwanzo wa mwaka viwanja
viwili vya mpira vimefunguliwa ambavyo ni Arena Amazonas, Arena da
Baixada, Arena Pantanal na Arena Corinthians, ambavyo karibia viko
tayari. Wakati Kombe la dunia likianza viwanja vyote vitakuwa
vimeshafanyiwa matukio ya majaribio. Haya yote ni muhimu sana ili
waandaaji waweze kufanya marekebisho ya mwisho katika mipango yao.
Hatuna muda mwingi wa kutosha mpaka mashindano yatakapoanza, na
wachezaji wakubwa katika sayari kwenda kifua mbele kama, Messi,
Christiano Ronaldo, Iniesta, Neymar…..siwezi kungojea. Ninawatarajia
nchini Brazil. Tutaonana katika Kombe la dunia.
No comments:
Post a Comment