Msemaji
wa maafande wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ametamba kuwa klabu yao
imejiandaa vizuri kuwazamisha maafande wenzao kutoka kule jijini Arusha,
uwanja wa Mabatini Mkoani Pwani.
Shooting wameingia katika rekodi msimu huu wa 2013/2014 baada ya kufungwa mabao 7-0 na Yanga ya Dar es salaam katika dimba la Taifa.
Timu nyingine ambazo zimekula kipigo kikali ni JKT Ruvu waliofungwa mabao 6-0 na Prisons.
Mgambo JKT walifungwa 6-0 na Simba mzunguko wa kwanza, huku Ashanti nao wakila kipigo cha 5-1 kutoka kwa Yanga.

HALL AKIRI LIGI KUU MSIMU HUU NI BORA, APONDA UBABAISHAJI WA VIONGOZI SOKA LA BONGO!!
Kocha wa Zamani wa Timu ya Taifa ya Zanzibar na Azam fc, Sterwart John Hall
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976 au 0764302956
WAKATI
ligi kuu soka Tanzania bara ikiwa wakati wa magharibi kwa maana ya lala
salama, aliyekuwa kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Zanzibar,
Zanzibar Heroes na klabu ya Azam fc mpaka mwishoni mwa mzunguko wa
kwanza msimu huu wa 2013/2014, Mwingereza Sterwart John Hall amesema
msimu huu una ushindani mkubwa zaidi ya msimu uliopita.
Katika
mahojiano maalumu na mtandao huu, Hall alisema imekuwa jambo zuri
kuibuka kwa timu ngumu kama Mbeya City, lakini bado kuna timu dhaifu
nyingi kitu ambacho si kizuri katika ligi.
“Nikiwa
kocha wa mpira, lazima nisema ukweli, msimu huu umekuwa bora zaidi,
lakini nadhani yanahitajika maboresho zaidi kwa klabu ili kupunguza
udhaifu wa timu nyingi”. Alisema Hall.
Kocha
huyo aliongeza kuwa imekuwa ikishangaza sana na ni jambo zuri pale timu
ndogo zinapotoa changamoto kubwa uwanjani dhidi ya timu kubwa za
Simba, Yanga na Azam fc.
“Zinahitajika
timu nyingi zenye ubora kama Mbeya City, hapo utaona ligi bora. Kuna
timu za chini, hakika zimekuwa zikionesha kiwang duni sana na kuharibu
utamu wa ligi”. Alisema Hall.
No comments:
Post a Comment