Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatafakari hatua zaidi za kinidhamu
dhidi ya wachezaji wawili wa kikosi cha Twiga Stars walioondolewa kwenye
timu hiyo na Kocha Rogasian Kaijage.
Kocha
Kaijage aliwatimua kambini wachezaji Mwapewa Mtumwa na Flora Kayanda
kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu wakati Twiga Stars ikijiandaa
kwa mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya
Zambia.
Twiga
Stars ilipoteza mechi ya kwanza ugenini mabao 2-1 na kutoka sare ya bao
1-1 katika mechi ya marudiano iliyochezwa Februari 28 mwaka huu Uwanja
wa Azam Complex, hivyo kutolewa katika mashindano hayo kwa jumla ya
mabao 3-2.
TFF
tunaunga mkono hatua iliyochukuliwa na Kocha Kaijage dhidi ya wachezaji
hao wakongwe wa Twiga Stars, kwani katika shughuli yoyote ile
inayohitaji ufanisi nidhamu ni kitu cha kwanza.
Twiga
Stars itacheza mechi za mchujo za michezo ya 11 ya Afrika (All Africa
Games) ambayo itafanyika mwakani nchini Congo Brazzaville.
No comments:
Post a Comment