CHADEMA JIMBO LA CHALINZE
TAARIFA KWA UMMA
Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Chalinze kimeanza mchakato wa ndani wa
kupata mgombea ubunge kwa ajili ya uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika mapema
mwezi Aprili, mwaka huu, ambapo fomu za uteuzi zimeanza kutolewa kwenye Ofisi Jimbo,
kuanzia tarehe 4 Machi na mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu hizo itakuwa tarehe
7 Machi 2014, saa 10.00, jioni.
Kura za maoni ndani
ya chama, zitafanyika tarehe 8 Machi katika Mji wa Chalinze na kufuatiwa na kikao
cha kamati ya utendaji ya jimbo ili kufanya uteuzi wa awali kwa mujibu wa Katiba
ya chama na hatimaye kikao cha Kamati Kuu kufanya uteuzi wa mwisho ili kupata mgombea
atakayeshindana na wagombea wa vyama vingine.
Mpaka sasa wagombea
waliochukua fomu kwenye ofisi ya jimbo ni watatu (3) na wagombea wengine watatu
(3) wamechukulia fomu Ofisi za Makao Makuu ya Chama, Dar es Salaam, hivyo hadi
sasa idadi ya wagombea waliotambuliwa rasmi ni sita.
Tunatumia nafasi
hii kuujulisha umma wa Watanzania, hususan wanachama wa CHADEMA, kuwa fomu za
kuwania uteuzi wa ndani zinaendelea kupatikana sehemu tatu, Makao Makuu ya
Chama, Ofisi ya Jimbo la Chalinze na kwenye tovuti ya chama www.chadema.or.tz
Imetolewa Machi 5, 2014
Iddi Omary Ucheche
Katibu wa CHADEMA, Jimbo la Chalinze
No comments:
Post a Comment