- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MKAZI MMOJA WA JIJINI MBEYA AKIWA MALI IDHANIWAYO KUWA YA WIZI.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
- MTU MMOJA MKAZI WA JIJINI MBEYA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA JIJINI MBEYA KWA KOSA LA KUFANYA BIASHARA BAADA YA MUDA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MKAZI MMOJA WA JIJINI MBEYA AKIWA MALI IDHANIWAYO KUWA YA WIZI.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA YONA MWANJELA (29) MFANYABIASHARA, MKAZI WA NZOVWE AKIWA NA MAFUTA
YA DIESEL MAPIPA MAWILI NA NUSU [2 ½] MADUMU 38 KILA DUMU LIKIWA NA
UJAZO WA LITA 20 JUMLA YA MAFUTA YOTE NI UJAZO WA LITA 1,260 MALI
IDHANIWAYO KUWA NI YA WIZI. MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 03.03.2014
MAJIRA YA SAA 15:30HRS ALASIRI HUKO KATIKA ENEO LA NZOVWE, KATA YA
NZOVWE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUMFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHAMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA SHUGHULI HIZI KWANI NI VITUO VYA MAFUTA NDIVYO VYENYE LESENI YA
KUFANYA SHUGHULI HIZI. PIA NI HATARI KWA MAISHA YA WATU WANAOISHI MAENEO
YA KARIBU PA.LE ITOKEAPO AJALI YA KULIPUKA. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO
KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA
MAENEO YAO KWA JESHI LA POLISI JUU YA SHUGHULI WANAZOFANYA ILI WAWEZE
KUFUATILIWA KWA KARIBU ZAIDI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
MWANAMKE
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA VICTORIA SEMPONDA (50) MFANYABIASHARA,
MKAZI WA MAFIATI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA
POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO [05]. MTUHUMIWA
ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 03.03.2014 MAJIRA YA
SAA 13:15HRS MCHANA HUKO KATIKA ENEO LA MAFIATI, KATA YA MAANGA, TARAFA
YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHAMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA
KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI
KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA KWA
JESHI LA POLISI/MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA
UTENGENEZAJI/USAMBAZAJI/UUZAJI WA POMBE HARAMU YA MOSHI ILI WAKAMATWE NA
HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
MTU MMOJA MKAZI WA JIJINI MBEYA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI.
MWANAUME
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NOAH ANTHONY (26) MFANYABIASHARA, MKAZI
WA ILEMI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI
KETE MOJA SAWA NA UZITO WA GRAM 05. MTUHUMIWA HUYO ALIKAMATWA MNAMO
TAREHE 03.03.2014 MAJIRA YA SAA 13:00HRS MCHANA HUKO KATIKA ENEO LA
MAFIATI, KATA YA MAANGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHAMED Z. MSANGI ANATOA
WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA KULIMA/KUSAMBAZA/KUUZA DAWA
HIZO ZA KULEVYA AZITOE KWA JESHI LA POLISI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA
KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA JIJINI MBEYA KWA KOSA LA KUFANYA BIASHARA BAADA YA MUDA.
MFANYABIASHARA
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FAUSTINE CHENGULA (28) MKAZI WA NZOVWE
NA WENZAKE WATANO [05] WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
WAKIWA WANAFANYABIASHARA YA POMBE BAADA YA MUDA KUISHA. WATUHUMIWA KWA
PAMOJA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 04.03.2014 MAJIRA YA SAA 01:05HRS USIKU
WA KUAMKIA LEO HUKO KATIKA ENEO LA NZOVWE, KATA YA NZOVWE, TARAFA YA
IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHAMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
WAFANYABIASHARA KUFUATA NA KUZINGATIA TARATIBU ZA KUENDESHA/KUFANYA
BIASHARA ZAO ILI KUJIEPUSHA NA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment