Katika kusheherekea siku ya wanawake duniani mwaka 2014. Sherehe rasmi zitafanyika katika mkoa wa Tanga
TFF
/TWFA wanaamini kuwa ili kuwa na kiwango kizuri na maendeleo katika
mpira wa miguu wanawake ni lazima kuanza na vijana wadogo hivyo basi
Shirikisho na chama cha mpira wa miguu Tanga limeandaa mafunzo kwa
walimu wapatao 30 toka shule15 za mkoa wa Tanga.
Walimu
hao watapatiwa mafunzo kwa siku mbili na tarehe 08/03/2014 kutakuwa na
Tamasha la Grassroot litakalojumusha jumla ya wanafunzi wapatao 1000
toka shule husika.
Ni
matumaini ya shirikisho kuwa mafunzo hayo na tamasha la grassroot
litaleta mwamko wa mpira wa miguu katika mkoa wa Tanga na hamasa kwa
watoto wa kike,wasichana na kina mama katika ushiriki wa mpira wa miguu
wanawake
No comments:
Post a Comment