Mjumbe
wa Baraza Kuu la Taifa la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha
Mapinduzi (UVCCM) kutoka Mkoa wa Tanga Ndugu Husna Mbwambo Sekiboko
amefunga tawi la Chadema katika Kijiji Cha Lukozi na kupandisha Bendera
ya Chama Cha Mapinduzi kutangaza Ufalme mpya wa Chama hicho cha siasa.
Tukio hilo limetokea jana tarehe 6th March
2014 katika kijiji cha Lukozi, wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga, ambapo
sambamba na kuasisi tawi hilo la Chama Cha Mapinduzi pia kiongozi huyo
wa UVCCM ameingiza wanachama wapya 206 ambapo wengi wao walikuwa ni
wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Mjumbe
huyo wa Baraza Kuu la Taifa la UVCCM, alifungua mashina sita yakiwemo
ya Manyara, bodaboda, n.k pia alifanya vikao vinne vya ndani ambapo
alizungumza na wanaCCM juu ya hali ya Uimara wa Chama na kuhoji kasi ya
utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Kijiji hicho ndani ya
Wilaya ya Lushoto pamoja na kufanya mkutano wa hadhara ambao
ulihudhuriwa na wananchi wengi wa Lukozi.
Pamoja
na vikao hivyo lakini pia Husna alitembelea vikundi vya ujasiriamali
vya akinamama pamoja na kambi ya JUDO ya Vijana wilayani Lushoto na
kujadili nao Changamoto wanazokutana nao na kushirikiana nao kuzipatia
ufumbuzi.
Husna
anafanya ziara za kawaida katika Mkoa mzima wa Tanga katika kuhamasisha
Vijana kujiunga na Chama Cha Mapinduzi pamoja na Jumuiya ya Umoja wa
Vijana.
No comments:
Post a Comment