WAJUMBE
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
jana jijini Dar es Salaam walivutiwa na teknolojia mpya inayotumiwa kwa
sasa na Shirika hilo katika utengenezaji wa kadi ya mwanachama wa NSSF.
Teknolojia hiyo mpya (mobile POS) ya utengenezaji wa kadi ya mwanachama
wa NSSF imerahisisha maradufu muda wa awali wa utengenezaji wa kadi ya
mwanachama (smart card) kutoka takribani wiki moja hadi ndani ya saa
moja kwa sasa.
Wakitembelea
miradi mbalimbali ya NSSF jana jijini Dar es Salaam Wajumbe wa Bodi ya
Wakurugenzi ya NSSF walishuhudia teknolojia hiyo katika Tawi la NSSF
Temeke, ambapo walishuhudia wateja wakihudumiwa na kupata kadi ya
uanachama wa taasisi hiyo ndani ya saa moja tofauti na ilivyokuwa awali.
Akiwaelezea
Wajumbe wa Bodi, Meneja Kiongozi wa NSSF Temeke, Yahaya Mhamali, ambapo
teknolojia hiyo inatumika tangu mwishoni mwa mwaka jana, alisema
imeboresha shughuli za huduma kwa wateja kwani kwa sasa mteja anapata
kadi ya uwanachama ndani ya saa moja tofauti na awali ambapo ilichukua
takribani wiki moja kabla ya mteja kupata kadi hiyo.
Alisema
teknolojia ya ‘Mobile POS’ kwa sasa inawawezesha NSSF kwenda moja kwa
moja na kifaa hicho ofisi walipo wateja wao na kuingiza taarifa za
mtena, kuzihakiki na hata kutoa kadi ya mwanachama huyo kwa muda mfupi
tofauti na ilivyokuwa awali.
Alisema kwa wateja wanaokuja
wenyewe ofisini na kuwa na taarifa zao hutengenezewa kadi ya uanachama
ndani ya saa moja jambo ambalo limeongeza ufanisi kihuduma tofauti na
ilivyo kuwa hapo awali. “…Sasa hivi mteja akija mwenyewe ofisini akiwa
na taarifa zake sahihi anapata kadi yake ndani ya saa moja na kuondoka,”
alisema Mhamali.
Wajumbe
hao walishuhudia mmoja wa wateja aliyetambulika kwa jina la Ester
Msalahi, ambaye ni mwalimu katika shule moja ya msingi ya binafsi
akihudumiwa na kupatiwa kadi yake ya uanachama ndani ya saa moja, ambapo
kadi hiyo ilikabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF,
Abubakar Rajabu huku akishughudiwa na wajumbe wa bodi na viongozi
waandamizi ya shirika hilo katika ziara hiyo.
NSSF kwa sasa inatumia mfumo wa
kompyuta wa kuwahudumia wateja katika ofisi hiyo ambapo mteja uchukuwa
tiketi ya huduma katika mashine maalumu ambapo itampa maelekezo eneo
analopaswa kuhudumiwa kwa wakati na kufuata utaratibu.
Aidha viongozi waandamizi wa NSSF
walitembelea jengo jipya la NSSF linalojengwa eneo la Ilala ambalo
litakuwa na ghorofa 20 kwenda juu huku likiwa na eneo la kuegesha magari
la ghorofa nne ardhini. Ghorofa hilo linalojengwa kisasa ambalo
litakuwa likitumiwa na NSSF Mkoa wa Ilala pia litakuwa na ofisi za
kukodi, kumbi za mikutano benki na huduma zingine za kawaida za jamii
mjini.
Akifafanua kwa wanahabari
kuhusiana na ujenzi wa jengo hilo, Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John
Msemo alisema jingo hilo kwa sasa limefikia hatua za mwisho kukamilika
kwani mafundi wanafanya matengenezo ya mwisho ili kumalizia ujenzi huo.
“…Jengo hili lipo katika hatua za
mwisho kukamilika, sehemu kuwa ya ujenzi imemalizika na kinachofanyika
sasa ni kuweka miundombinu kama ya maji, umeme na vutu vingine kama
hivyo. Ghorofa hili pia kutakuwa na maeneo ya kupangisha wateja kwa
shughuli mbalimbali…,” alisema Msemo.
Akifafanua zaidi Mhandisi Msemo alisema ujenzi wa ghorofa hilo la kisasa umegharimu shilingi za Kitanzania bilioni 40.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment