BARAZA
la madiwani Meru lenye jumla ya madiwani 23 limeathimia kujiuzulu
nyadhifa hiyo ya udiwani endapo kama Serikali haitaweza kuingia kati
masakata mbalimbali ya migogoro ya radhi iliyodumu kwenye halmashauri
hiyo kwa muda mrefu
Uamuzi
huo uliwekwa hadharani juzi mara baada ya kumalizika kwa baraza la
madiwani lililofanyika katika halmashauri ambapo lilitoa siku chache kwa
serikali kuweza kuingilia kati.
Akiongelea
sakata hilo mmoja wa madiwani wa Halmashauri hiyo loti Nnko alisema
kuwa sakata la migogoro ya ardhi kwenye halmashauri hiyo limedumu kwa
muda mrefu sasa ndio maana wwamefikia uamuzi wa kutaka kujiengua katika
nyadhifa hiyo ya udiwani.
Nnko
alisema wanachokisubira kwa sasa ni majibu kutoka kwa kamati ambayo
wameiunda ambapo kamati hiyo itaenda Jijini Dar es saalam wiki ijayo na
watakaporudi basi watarudi na majibu ambayo yataweza kuwafanya kuondoka
kwenye viti hivyo vya udiwani.
Akitolea
mfano moja yashamba lenye migogoro katika Halmashauri hiyo,shamba la
Madira lililopo katika maeneo ya Seela Singisi ambalo ni mali halisi
ya Halmasahuri hiyo lakini kwa sasa kuna migogoro ambayo inasababishwa
na baadhi ya viongozi jambo ambalo wamedai kuwa hawataweza kuvumilia
bali wataingia katika vita kwa mara nyingine
“kwa
mfano hili shamba la Seela Singisi ni mali ya wananchi wote wa Meru na
hadi Raisi ameshaweka saini yake jamani litumike kwa ajili ya matumizi
ya kata zote za Meru lakini vigogo wanasema ni mali yao alafu bado
tumenyamaza tu haitawezekana tunaachia udiwani alafu htunaingia katika
Vita kwa mara nyingine”aliongeza Kimu.
“hili
ni tamko rasmi tunatoa tunataka majibu ya migogoro hii rasmi kama
hatupewi itakuwa ni vita baina ya Wameru na hawa wanaojichukulia ardhi
kinyemelea, pia itakuwa ni huzuni kubwa kwa CCM manake kwanza sisi wote
hapa tunatokea CCM uzalendo umetushinda kabisa”aliongeza Nyiti
Naye
Mwenyekiti wa Halmasahuri hiyo ya Meru, Goodson Majola alisema kuwa
tamko hilo la kutaka kujiuzulu kwa madiwani 23 wote wa halmashauri hiyo
lipo sawa kabisa kwa kuwa migogoro yote ya ardhi inasababishwa na
Viongozi wasio waadilifu kuanzia ngazi ya Halmashauri hadi Wizara
“mimi
nasema kuwa tutajiuzulu wiki chache zinazokuja baada ya kujiridhisha
juu ya maangaiko haya ya ardhi ambayo yamedumu toka karne hadi karne na
ninasiistiza kuwa itakuwa ni kilio kwa CCM kwa kuwa wanchama wetu nao
tutaweka chini ya ulinzi hadi tutakapowaambia hawatajishugulisha na
shuguli yoyote ya chama”alisema Majola.
Majola
alisema kuwa kujiuzulu kwao lakini pia kuondoka na wanachama wote wa
CCM katika Wilaya hiyo ni uzalendo wao kwa wananchi na hivyo Hata CCM
nao hawapaswi kuumia kwa hilo.
No comments:
Post a Comment