Young
Africans ambao ndio wawakilishi pekee wa mashindano ya kimataifa nchini
Tanzania kawa sasa walishuka dimbani kwa lengo moja tu la
kuhakikisha historia inaandikwa kwa kuvunja mwiko dhidi ya Waarabu na
kuibuka na ushindi katika mchezo huo.
Kikosi
cha Mholanzi Hans Van de Pluijm baada ya kujifua na mazoezi asubuhi
na jioni katika Uwanja wa Boko Beach kujiandaa na mchezo huku morali ya
wachezaji ikiwa i ya hali ya juu, saikolojia na kimwili wakiwa tayari
kwa mechi walifanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0.
National
Al Ahly ambao waliwasili jumatano asubuhi majira ya saa 10:00
jioni walifanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa tayari kwa kuuzoea kwa
mchezo kufuatia kufanya mazoezi kwa siku mbili katika shule ya
IST Upanga.
No comments:
Post a Comment