BARAZA
la Sanaa la Taifa (BASATA) mwishoni mwa wiki iliyopita lilikabidhi
kibali kupitia Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Godfrey Mngereza kwa
ajili ya uendeshaji wa Tamasha la Pasaka linaloandaliwa na Kampuni ya
Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam.
Tamasha
hilo ni muendelezo wa Tamasha la Pasaka lililoasisiwa tangu mwaka 2000
likiwa na lengo la kumtukuza na kumtumikia Mungu kupitia nyimbo
mbalimbali za waimbaji wa Tanzania na nje ya nchi.
Akizungumza
na gazeti hili Mratibu wa tamasha hilo ambaye pia ni mjumbe wa Basata
Alex Msama, alisema kibali kilitolewa wiki iliyopita kwa ajili ya
tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Aprili 20, jijini Dar es Salaam
kabla ya kuhamia katika mikoa nane itakayochaguliwa kufanyika kwa
tamasha hilo kupitia mfumo wa upigaji kura kupitia ujumbe mfupi wa
maandishi.
Msama
alisema taratibu za maandalizi ya tamasha hilo zinaendelea ikiwa ni
pamoja na waimbaji kupigiwa kura na kufanya mazungumzo na wale
watakaoshinda kwa kupigiwa kura nyingi ndio watakaotumbuiza na pia
kupata mahali litakapofanyika.
“Maandalizi
kwa ujumla yanaendelea vizuri kabisa, kibali kimepatikana
kinachoendelea sasa ni kwamba tumewapa nafasi watanzania wenyewe
wachague mgeni rasmi na waimbaji wataoimba katika tamasha la mwaka huu,
kwa mgeni rasmi tunaomba waendelee kupiga kura kwa wingi ili kuchagua
mahitaji hayo,” alisema Msama.
Msama
amendelea kuwakumbusha watanzania namna ya kuwapigia kura waimbaji,
mgeni rasmi na mikoa ambako ukitaka kumpigia mwimbaji andika pasaka acha
nafsi kisha andika jina la mwimbaji unatuma kwenda namba 15327.
Pia
kwa mgeni rasmi andika neno pasaka acha nafasi kisha andika jina la
mgeni rasmi unayetaka kumpigia kura tuma kwenda 15327, wakati mikoa
unaandika pasaka acha nafasi jina la mkoa unaotaka kuupigia kura tuma
kwenda namba 15327 piga kura uwezavyo ili upate mwimbaji na mgeni rasmi
na mkoa unaopenda tamasha lifanyike.a
No comments:
Post a Comment