Wanafunzi
wa Kitanzania nchini Thailand, wakiwa katika picha ya pamoja na
wanafunzi wenzao kutoka mataifa mbalimbali , ambao wamelitembelea banda
la Tanzania. Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini katika picha ya pamoja na wanafunzi hao katika banda la Tanzania.
……………………………………………………………………………………
Na Asteria Muhozya, Bangkok
Wanafunzi
wa Kitanzania wanaosoma masomo ya Geomolojia katika Chuo cha ‘Asian
Institute of Geological Science’ (AIGS) nchini Thailand, wamewataka
wadau wa tasnia ya madini ya vito na usonara nchini Tanzania kuichukua
sekta hiyo kwa umakini mkubwa kutokana na mchango wake kiuchumi.
Aidha,
wameeleza kuwa, nchi ya Thailand imepiga hatua kubwa katika sekta ya
madini ukilinganisha na Tanzania lakini bado Tanzania inaweza kufaidika
zaidi katika sekta hiyo ikiwa kila mdau atatimiza wajibu wake kikamilifu
ili madini ya vito yaongeze mchango katika pato la taifa.
Wameongeza
kuwa, Tanzania bado ina nafasi ya kujipanga upya kuhusu kuboresha zaidi
sekta hiyo kama ilivyo kwa nchi nyingine endapo mipango mikakati ya
maboresho itatekelezwa na kusimamiwa kikamilifu.
Wanafunzi
hao wameyasema hayo, wakati walipolitembelea banda la Tanzania katika
maonesho ya 53 ya Vito vya Usonara na Madini yanayoendelea katika jiji
la Bangkok ambapo nchi zaidi ya 150 zinashiriki maonesho hayo.
“Thailand
wamejipanga vizuri katika sekta ya madini. Wafanyabiashara wa madini
wana umoja. Wadau wa madini wanatakiwa kuelewa kuwa madini
yanawakilisha utajiri wetu tulionao”. Amesema Agatha Mwinuka.
Aidha,
wameitaka serikali na wadau wa Tanzania wanaoshiriki maonesho hayo
kujifunza kutokana na changamoto wanazozipata kutoka kwa nchi nyingine,
jambo ambalo litasaidia kuboresha sekta ya madini na vito, ikiwa ni
pamoja na wafanyabiashara kuhakikisha kuwa wanafuata sheria na taratibu
zilizopo.
“Tunaiomba
serikali iendelee kuendeleza viwanda vya kukata madini. Ni jambo zuri
kama shughuli hizi za kukata madini zitafanyika ndani ya nchi badala ya
nje. Jambo hili linasaidia sana kuongeza thamani ya madini. Ameongeza,
Emmanuel Minja.
Akiongelea
kuhusu umuhimu wa kuendeleza na kuboresha kituo cha Tanzania
Geomological Center, Doricas Moshi, ameeleza kuwa, kituo hicho
kinaweza kutoa mchango mkubwa katika tasnia hii hasa katika nyanja ya
ukataji madini na uthamini wa madini hivyo, ameitaka Serikali
kukiongezea nguvu kituo hicho kutokana na umuhimu wake kwa maendeleo ya
Tanzania.
“Chuotunachosoma
hapa kinatumia sana mifano ya madini ya Tanzania katika kufundisha.
Mengi yametoka nyumbani, hii ni ishara nzuri. Serikali iliangalie hili.
Ameongeza Doricas.
Aidha,
wameeleza kuwa, soko la kimataifa kwa madini ya Tanzania lipo, hivyo,
wamewataka wadau wote kuhakikisha wanashirikiana vizuri na serikali
kuendeleza sekta hiyo kutokana na umuhimu na mchango wake kwa taifa.
Akizungumzia
mipango iliyopo ya kuboresha sekta hiyo, Kamishna Msaidizi wa Madini,
Mhandisi Hamis Komba, amesema kuwa, Serikali kupitia Shirika la Madini
Tanzania (STAMICO), inatekeleza mikakati ya kuwasaidia wachimbaji wadogo
na wa kati ili waweze kuendana na mahitaji ya soko la kimataifa kwa
kuwapatia mafunzo mbalimbali yakiwemo ya kukata madini, kuyaongezea
thamani na kuwapatia mikopo kupitia Benki ya TIB.
“STAMICO
imepewa jukumu la kuwaendeleza wachimbaji wadogo katika sekta ya madini
hususani katika masuala ya uchimbaji, uongezaji thamani madini na
biashara ya madini. Serikali imejipanga vizuri katika hilo”. Ameongeza
Kamishana.
Ameongeza
kuwa, Serikali inatambua kwamba wachimbaji wengi wapo katika sekta ya
madini ya vito na usonara hivyo, jitihada za kuwaendeleza zitasaidia
kufikia kiwango bora cha utendaji wao wa kazi.
Vilevile,
ameongeza kuwa, kutokana na kuboreshwa kwa Sheria ya madini ya mwaka
2010 ambayo inaiwezesha STAMICO kumiliki asilimia 50 ya hisa katika
mgodi wa Tanzanite One, jambo ambalo linaifanya Serikali kuwa mmiliki
katika mgodi huo.
No comments:
Post a Comment