Afisa
mnadhimu wa Polisi Kinondoni SSP Bibie Juma akikabidhiwa msaada wa
samani za Ofisi na afisa usiano na matukio wa kampuni ya mawasiliano ya
airtel Dangio Kaniki.
………………………………………………………………………………
Na Abdallah Selemani wa Jeshi la Polisi.
Kampuni
ya mawasiliano ya simu airtel Tanzania imetoa msaada wa samani za
ofisi,vikiwemo viti sita na meza sita kwa jeshi la polisi mkoa wa
Kipolisi Kinondoni.
Msaada
huo ni kwa ajili ya matumizi ya ofisi za kikosi cha usalama barabarani
mkoa wa Kinondoni ambazo zitapelekea kuwaongezea ufanisi askari wa
usalama barabarani .
Akikabidhi
samani hizo machi 5 katika viwanja vya polisi oysterbay afisa usiano
na matukio wa kampuni ya mawasiliano ya airtel Dangio Kaniki alisema
wamekabithi misaada kwa lengo la kukuza ushirikiano kati ya jeshi la
polisi na kampuni ya airtel.
Dangio kwa niaba ya airtel ameidi kuendelea kutoa misaada kwa jeshi la polisi kadri wawezavyo.
Akizungumza kwa
niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni afisa mnadhimu wa polisi
kinondoni(SSP) Bibie juma athumani alisema anaishukuru kampuni ya
airtel kwa msaada waliotoa na kuahidi kutunza samani hizo na kutoa wito
kwa makampuni mengine ya mawasiliano kulisaidia jeshi la polisi.
No comments:
Post a Comment