Bw.Carl
Davis Jr, Rais wa Silicon Valley Black Chamber of Commerce na Eng.
George Mulamula, Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi (kulia) wakisaini MOU.
Na Mwandishi Wetu, MOblog Tanzania
KAMPUNI
tanzu ya Tume ya sayansi na teknolojia ya DTBi-COSTECH na Silicon
Valley Black Chamber of Commerce’s Center for Entrepreneurial
Development (SVCED) wametiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano (MoU)
ambapo pande zote mbili zitashirikiana kwa njia mbalimbali kwa ajili ya
ukuaji wa wajasiriamali.
Mkataba
huo, kati ya DTBi na SVCED utawezesha pande hizo mbili kukuza
ujasiriamali na kujenga uwezo katika Habari, Teknolojia na Mawasiliano
kwenye sekta zote za kiuchumi.
Mkataba
huo wa MoU utawafanya wadau kufanya shughuli za biashara kwa kuanza na
mfumo wa teknolojia ya habari na mawasiliano kwa kupitia njia ya mtandao
na kusaidia wale walio na ubunifu katika nyanja mbalimbali za biashara.
Bw.
Carl Davis Jr, Rais wa Silicon Valley Black Chamber of Commerce na Eng.
George Mulamula, Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi kupeana mikono baada ya
kusaini MOU.
Mkataba
huo pia utasaidia wajasiriamali kuweza kukua na kufanya biashara kwa
kutumia mifumo habari, teknolojia na mawasiliano katika kukuza
ujasiriamali na kuanzisha mfumo wa kubadilishana uzoefu katika
kuendeleza biashara na ukuaji wa ujasiriamali.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi, Injinia. George Mulamula
amesema mkataba MOU utatoa ushirikishiano ambao utaruhusu wajasiriamali
wa Tanzania kufaidika na ujuzi, maarifa ya Silicon Valley ya
ujasiriamali.
Amesema
hii itasaidia nchi ya Tanzania kuruhusu uanzishwaji wa biashara kupitia
njia ya mtandao na mifumo ya Habari, teknolojia na mawasiliano katika
kukuza ajira na kuchangia pato la taifa.
Eng.George Mulamula akielezea ushirikiano kwa vyombo vya habari.
Baada
ya kutiliana saini ya MOU, Bw Carl Davis Jr, alikuwa na semina kwa
wajasiriamali yenye jina la “The Mindset of the Silicon Valley
Entrepreneur: Lessons for the Tanzania Entrepreneur/Innovator”.
Mr
Davis Jr amesema anaweza kuwasaidia “wajasiriamali kuelewa jukumu la
uzinduzi na ujasiriamali na jinsi Wajasiriamali hapa nchini jinsi
wanavyoweza kujiinua katika kufikiri chanya kwenye maeneo ya biashara.
Bw. Carl Davis Jr, akitoa majadiliano DTBi kwa wajasiriamali wa Tanzania juu ya jinsi ya kuwa mwekezaji mwenye mafanikio.
Mshiriki akichangia mjadala.
No comments:
Post a Comment