Ujumbe kabla ya kifo: Kijana aliyejichinja ndani ya basi akiandika ujumbe kabla ya kukata roho.
duniani
kuna mambo kwani dereva na abiria wa basi la Manchester ambalo namba
yake haikujulikana mara moja, lililokua likitoka Lindi kwenda jijini Dar
es Salaam walijikuta wakiangua vilio baada ya kumuona mwenzao
akijichinja hadi kufa kwa kisu ndani ya gari hilo. Kwa
mujibu wa chanzo, tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa tisa alasiri,
Jumatano wiki iliyopita mara basi hilo lilipofika katika hoteli moja ya
Nangulukulu kwa ajili ya kupatia chakula.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki iliyopita, baadhi ya abiria walioshuhudia tukio hilo
walisema kuwa mara walipofika katika hoteli hiyo, kila mmoja
alitawanyika kwa lengo la kujipatia chakula na baadhi yao walienda
maliwatoni akiwemo marehemu huyo.
Walisema
kwamba marehemu huyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja, wakati
wa kushuka hakuonekana na kisu aina ya sime lakini baadaye abiria
wachache waliotangulia kwenye gari, walimshuhudia akiwa ameshika sime
hiyo mkono pasipokujua aliipata wapi.
“Hata
sisi tulishangaa kumuona akiwa karibu na usukani wa dereva huku
akizamisha sime tumboni kisha kuichomoa na kujichinja shingoni hadi
pale alipokuwa akivuta koromeo na kuning’inia.
Damu kila mahali: ...Akiingizwa katika gari lingine huku damu zikiwa zimetapakaa.
“Tulichanaganyikiwa
kwani ni kitu ambacho hatukukitarajia na wala hatujawahi kushuhudia
tukio kama hilo la mtu kujichinja hadharani, tulibakia kutokwa machozi
huku akina mama wakipiga yowe, hakuna mtu aliyethubutu kumsogelea
kumuokoa kwani kila mmoja alimuogopa.
“Tulishindwa
kupanda basi hilo kwani ni tukio la ajabu pia ndani kwa mbele kulikuwa
kumetapakaa damu, ghafla alidondoka chini ndani ya gari, aliomba kalamu
na karatasi ili kuandika ujumbe.
Silaha:Polisi akiwa na sime aliyotumia kujichinja kijana huyo.
“Dereva
alichukua kalamu na kipande cha karatasi na kumpa, alianza kuandika
huku damu ikimbubujika tumboni na shingoni, hatukujua alichokiandika,
aliishiwa nguvu taratibu akadondoka.
“Abiria
walimsogelea na kumuinua na walimueleza kuwa atubu kwa Mungu kosa
alilolifanya kabla hajafa, alipiga magoti na kuomba, ghafla alidondoka
tena.
Imani:Kijana akisali kabla ya kukata roho.
“Kaka
yake ambaye alikuwa akisafiri naye kuelekea Dar es Salaam
alichanganyikiwa kwani hakutegemea kuwa mdogo wake angejiua, kwani
alisema hana historia ya kuugua ugonjwa wa akili. Polisi walipigiwa simu
na walifika kumchukua lakini baada ya muda mfupi akawa amefariki dunia.
“Sisi abiria wengine tuliendelea na safari kuelekea Dar es Salaam ambapo marehemu na kaka yake walibakia huko mkoani Lindi.
“Mara
tulipofika Dar es Salaam dereva alitusihi tukae kimya kwa dakika moja
na kuomba kutokana na tukio lililotupata, tulifanya hivyo baadaye kila
mmoja alitawanyika na kuelekea kwake,” kilisema chanzo kwa sharti la
kutoandikwa jina gazetini.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Lindi, ACP Renatha Mzinga alipoulizwa mwishoni mwa
wiki iliyopita kuhusiana na tukio hilo alikiri kutokea.
“Ni kweli tukio hilo
lilitokea lakini kwa sasa sina data kwani nipo njiani nikitokea Nairobi,
Kenya kikazi kuelekea Lindi, mara nitakapofika huko ofisini ndipo
nitapata tukio zima lilivyokuwa,” alisema Kamanda Mzinga
No comments:
Post a Comment