Kaimu
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la ATCL, Kapteni Milton Lazaro
(kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo mara
baada ya kuwasili kwa ndege mpya ya shirika hilo aina ya CRJ-200,
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam Alhamis usiku. Kaimu
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la ATCL, Kapteni Milton Lazaro
(Kulia) akiwatambulisha baadhi ya watendaji wa shirika hilo mara baada
ya kuwasili kwa ndege mpya ya shirika hilo aina ya CRJ-200, katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Alhamis usiku. Wafanyakazi
wa Shirika la Ndege la Taifa Air Tanzania (ATCL) wakisheherekea mara
baada ya kuwasili kwa ndege mpya ya shirika hilo aina ya CRJ-200, katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Alhamis usiku. Picha
ya ndege mpya ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL), aina ya CRJ-200 ya
nchini Canada, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Alhamis usiku.
……………………………………………………………………………………………………………..
- Yaanza utekelezaji wa mkakati wa kuimarisha huduma zake
- Kupata ndege mbili mpya zenye uwezo wa kubeba abiria 78 ifikapo mwezi Mei
- Yaondoa adhabu na masharti magumu kwa abiria wanaobadilisha tarehe za safari na wanaochelewa kufika uwanjani siku ya safari
Na Mwandishi Wetu.
SHIRIKA
la Ndege la Taifa (Air Tanzania) limepata ndege nyingine aina ya
CRJ-200 ya nchini Canada yenye uwezo wa kubeba abiria 50, ikiwa ni
sehemu ya utekelezaji wa mkakati wake madhubuti wa kuimarisha huduma
zake.
Shirika
hilo la Air Tanzania (ATCL) linaona ujio wa ndege hii kama chachu ya
kutimiza azma yake ya kuimarisha huduma zake ikiwa ni pamoja na kuongeza
safari zake katika njia wanazoruka kwa sasa, kuanzisha njia nyingine
mpya, na kuwahakikishia wateja wake uhakika wa huduma zake.
Mara
tu baada ya ndege hiyo kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Alhamis usiku, Kaimu Ofisa Mtendaji
Mkuu wa ATCL, Captain Milton Lazaro alisema kuwa kuna matumaini makubwa
ya Shirika la Ndege la Taifa kufanya vizuri zaidi katika utoaji wa
huduma za usafiri wa anga, ikizingatiwa kuwa shirika lina mkakati
madhubuti wa upanuzi wa huduma zake ambao utekelezaji wake umeanza.
“Ndege
tuliyoipokea leo hii, ni sehemu ya ndege tatu tulizopanga kuleta mwaka
huu. Ndege nyingine mbili zinatarajiwa kufika kati ya mwezi Aprili na
Mei mwaka huu. Kuongezeka kwa idadi ya ndege zetu kutatuwezesha sisi
kufungua mipaka kwa kuanzisha njia mpya na kuongeza safari nyingi zaidi
katika maeneo tunayoenda kwa sasa,” alisema Kapteni Lazaro.
Alisema
kuwa ndege mbili zitakazoletwa nchini ifikapo Mei, zinauwezo wa kubeba
abiria 78 na ni toleo jipya katika sekta ya usafiri wa anga, na
zitatumika katika kusafirisha abiria ndani na nje ya nchi.
Kapteni
Lazaro alisema kuwa shirika lake linampango wa kuanzisha safari mpya
ikiwa ni pamoja na ya Tabora – Mpanda, Mbeya- Dar es Salaam na kuongeza
idadi ya safari za Mwanza- Dar es Salaam, Dar es Salaam-Comoros na
Mtwara pamoja na Kigoma.
“Kwa
ongezeko hili la safari zetu, abiria wetu watafurahia safari za kila
siku za kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, ikiwa muda wa kuondoka Dar
kuwa 1600hrs na kutoka Mwanza kuwa 1800hrs. Tutakuwa tukienda mkoani
Mbeya mara nne kwa wiki; kwa siku za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na
Jumapili. Wakati Moroni katika visiwa vya Comoro tutakwenda katika siku
za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi. Na pia tunategemea kuzindua
safari ya Tabora – Mpanda hivi karibuni,” alisema.
Aliongeza
kuwa shirika hilo pia limeondoa baadhi ya adhabu watozwazo abiria
endapo wanashindwa kusafiri siku na muda waliyoomba, na kusema kuwa hii
itawasaidia abiria wao kutoingia gharama za ziada endapo watakumbana na
dharura mbali mbali kabla ya safari.
“Katika
jitihada za kuwasaidia abiria wetu na kuwaonyesha kuwa tunayatambua
mazingira tunayoishi na yakibiashara vizuri, shirika limeamua kuondoa
adhabu kwa abiria ambao watashindwa kufika uwanja wa ndege kabla ya muda
wa ndege kuondoka na adhabu ya kubadilisha safari,” alisema Kapteni
Lazaro.
Kwa
mujibu wa Ofisa Mtendaji huyo, upatikanaji wa ndege hiyo utaongeza idadi
ya abiria kwa kati ya asilimia 30 mpaka 40, kutokana na kuwa huduma za
shirika hilo bado ni nzuri na viwango vya nauli ni vya kiushindani zaidi
na vyenye unafuu ukilinganisha na mashirika mengine.
Kwa
kutumia ndege yake aina ya Bombardier Dash-8, ATCL kwa sasa inasafiri
katika zaidi ya maeneo nane (8) nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na
Mtwara, Mwanza, Tabora, Kigoma, Dar es Salaam, Mbeya, Bujumbura na
Moroni nchini Comoro.
No comments:
Post a Comment