Moja
kati ya msanii anayefanya muziki wa bongo fleva Edson Wilison a.k.a
Baby boy ambaye alipotea kwenye game ya muziki,sasa amerudi kwa kishindo
kikali.
Baby
boy ambaye alipotea kwa kipindi kirefu, zaidi ya miaka miwili kwenye
muziki sasa amerudi na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Funga
Mkanda aliyofanya chini ya studio iliyopo maeneo ya sinza lego jijini
dar es salaam inaoitwa Flexible music.
Ngoma hiyo ambayo Baby Boy akiwa
amemshirikisha Barnaba boy na msanii anayeitwa Shazy Melody,ambaye yupo
lebo chini ya Flexible Entertainment ikiwa imetengenezwa na mtayarishaji
Basmart the next hit wa studio hiyo.
Baby Boy akizungumza kuhusu ujio
wake mpya ameeleza kuwa unampa matumaini sana na kuwaomba mashabiki wake
wampokee vizuri maana ndiyo amerudi kwa nguvu zote.
“Hii ni ngoma yangu mpya ambayo
nimefanya na Barnaba Boy na Shazy Melody na wimbo wangu unaitwa Funga
Mkanda ambayo natarajia kuiachia siku yangu ya birthday yaani siku yangu
ya kuzaliwa alhamisi ya tarehe 6 mwezi huu” Baby Boy alisema.
Pia aliongeza kuwa ujio wake huo hautaweza kumfanya arudi nyuma tena kwenye muziki na alifafanua kuhusu ngoma hiyo
“Aaah ni ngoma ambayo naelezea
jinsi gani nimerudi maana najua mashabiki zangu walikuwa na hamu na mimi
kwa kipindi kirefu sana kama mtu aliyekuwa na kiu jangwani”Aliongeza
Baby Boy.
No comments:
Post a Comment