Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akipewa maelezo kwa kutumia mchoro kuonesha mzunguko
mzima wa maeneo atakayotembelea katika kikosi cha Komando
ARIDHISHWA NA UTIMAMU WA VIKOSI HIVYO KIMAFUNZO NA ZANA
· AAHIDI TATIZO LA MAJI KUPATIWA UFUMBUZI NDANI YA MWAKA 2014
· KIKOSI CHA UHANDISI WA MEDANI CHAAHIDIWA VIFAA ZAIDI ILI KUPAMBANA NA MAJANGA NCHINI
· AAGIZA JWTZ KUBUNI MIKAKATI YA KUONDOKANA NA MAKAZI YA MUDA
Ziara
hiyo ya siku moja ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe.
Joel Bendera, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Wakuu wa
Kamandi, Wakuu wa Matawi Makao Makuu ya Jeshi, Makamishna Wizarani na
Wajumbe wa Mabaraza ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya na Mkoa wa Morogoro.
(Na Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na JKT)
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Kikosi cha Komando kuanza ziara yake ya
kujionea hali na utimamu wa vikosi vya JWTZ Mkoani Morogoro.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akipokea taarifa ya Utawala na Utendaji kivita kutoka kwa
Mkuu wa Kikosi cha Komando wakati wa ziara yake.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akiangalia kupitia kilengeo maalum kinachotumiwa kwenye
silaha na makomando kulengea shabaha.
Makomando
wakimuonesha Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayuko pichani) mapigano bila
shilaha wakati wa ziara yake.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akifurahia mapambano ya kareti, taikondo na judo
yaliyokuwa yakioneshwa na makomando wa JWTZ (Hawamo pichani).
Komando
wa JWTZ akionesha uwezo wa kukwepa mapigo ya risasi za adui kwa kupita
juu ya mapigo hayo kwa kutumia kamba na kisha kuendelea na jukumu
alilopewa.
Kamanda
wa Kikosi cha Uhandisi wa Medani akitoa taarifa ya Utawala na Utendaji
Kivita kwa (Hayupo pichani) mara baada ya Kikosi hicho kutembelewa.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akifafanua maeneo kadha ambayo Wahandisi Medani wa JWTZ
wamefanya kazi nzuri kurejesha miundombinu ya reli, barabara na madaraja
hata pale ambako Mamlaka za Kiraia zimekuwa na maoni kuwa kazi hizo
zingehitaji muda mwingi zaidi.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akipewa maelezo kuhusu moja ya mitambo mipya inaotumiwa
na Wahandisi medani kusafisha maji chumvi na baridi na kuwa maji safi na
salama inayomilikiwa na Kikosi cha Uhandisi Medani.
Akipata maelezo kuhusu baadhi ya mitambo mipya ya kutengeneza barabara katika Kikosi cha Uhandisi Medani.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akivuka juu ya daraja jipya la medani lililojengwa
kumuonesha uwezo wa Wahandisi Medani wa JWTZ kuendelea kusaidia
usafirishaji wa zana na vifaa hata pale madaraja ya kudumu
yanapoharibiwa kwa namna yoyote ile.
No comments:
Post a Comment