MANCHESTER
City chini ya kocha wake, Manuel Pellegrini imefanikiwa kutwaa Kombe
la Ligi, maarufu kama Capital One Cup kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya
Sunderland usiku wa jana Uwanja wa Wembely, London.
Man
City waliuanza vibaya mchezo huo baada ya kutanguliwa na Sunderland
kwa bao la Borini dakika ya 10 kabla ya kuzinduka kipindi cha pili na
kuwafumua Sunderland.
Wafungaji wa mabao ya City walikuwa ni Yaya Toure dakika ya 55, Samir Nasri dakika ya 56 na Jesus Navas dakika ya 90.
Baada
ya kutwaa kikombe hicho, sasa Man Pellegrini anapata la kuongea
kufuatia kufanya vibaya kwenye mashindano ya ligi ya mabingwa barani
Ulaya dhidi ya FC Barcelona, ambapo walilala mabao 2-0 kutoka kwa wakali
wa dunia, FC Barcelona na yeye kumshambulia refa na baadaye kufungiwa
mechi tatu.
Lakini
hakufanya vibaya pekee yake UEFA, hata, hata Arsene Wenger na David
Moyes walikula vipigo vya 2-0, huku Chelsea pekee kwa klabu kutoka
England ikiambulia sare ya bao 1-1 huko Uturuki.
Kikosi
cha Man City kilikuwa: Pantilimon, Zabaleta, Kompany, Demichelis,
Kolarov, Nasri, Toure, Fernandinho, Silva/Javi Garcia dk77,
Dzeko/Negredo dk88 na Aguero/Navas dk58.
Sunderland:
Mannone, Bardsley, Brown, O’Shea, Alonso, Ki, Larsson/Fletcher dk60,
Cattermole/Giaccherini dk77, Colback, Johnson/Gardner dk60 na Borini.
Mabingwa: Manchester City wametwaa taji la Capital One Cup kwa kuifunga Sunderland 3-1 kwenye fainali
Mfaransa mwenye kipaji kikubwa, Nasri akishangilia baada ya kufunga
Wachezaji wa Manchester City wakisherehekea Uwanja wa Wembley
Mbali na mcheo huo wa Capital one, ligi kuu soka nchini England iliendelea kwa mechi tatu kupigwa.
Tottenham
wakiwa nyumbani kwao walishinda bao 1-0 dhidi ya Cardif City. Bao pekee
la ushindi lilifungwa na Roberto Soldado akipokea pasi kutoka kwa
Emmanuel Adebayor.
Matokeo kwa ujumla yalikuwa hivi;
England: Premier League
Finished
|
|
1-0 |
Cardiff
|
(1-0) | |||||
Finished
|
|
1-1 |
Crystal Palace
|
(1-0) | |||||
Finished
|
|
4-1 |
Norwich
|
No comments:
Post a Comment