by John Bukuku on March 5, 2014 in JAMII
· NG’OMBE 30 WAIBWA KATIKA KIJIJI CHA STAMICO WILAYANI CHUNYA.
· MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI WILAYANI CHUNYA.
· JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU WAKIWA NA NOTI BANDIA.
· JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA MAFUTA – DIESEL MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI.
· JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA MAFUTA – DIESEL YANAYODHANIWA KUWA YA WIZI.
· WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU.
· JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LATEKETEZA SHAMBA LA BHANGI LENYE UKUBWA WA HEKARI MOJA WILAYANI CHUNYA.
· WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI.
NG’OMBE 30 WAIBWA KATIKA KIJIJI CHA STAMICO WILAYANI CHUNYA.
NG’OMBE
30 MALI YA MIHAMBO PAUL (34) MFUGAJI, MKAZI WA KIJIJI CHA STAMICO
WALIIBWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE
01.03.2014 MAJIRA YA SAA 17:00HRS JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA STAMICO,
KATA YA MKOALA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA WAKATI MIFUGO HIYO
IKIWA MALISHONI BILA MSIMAMIZI. THAMANI HALISI YA NG’OMBE HAO NI
TSHS.15, 000,000/=. MSAKO MKALI UNAFANYWA ILI KUWABAINI WALE WOTE
WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIOPO WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AU
MIFUGO HIYO AZITOE KWA JESHI LA POLISI/MAMLKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA
HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI WILAYANI CHUNYA.
MTU
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA VENANCE SERA (70), MKAZI WA KIJIJI CHA
UPENDO ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI ISIYOFAHAMIKA NAMBA
ZAKE ZA USAJILI ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA CHALYA KASEMA. AJALI HIYO
ILITOKEA MNAMO TAREHE 04.03.2014 MAJIRA YA SAA 18:00HRS JIONI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA UPENDO, KATA YA MAMBA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA
CHUNYA. MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA PIKIPIKI MARA BAADA YA TUKIO. JUHUDI ZA
KUMTAFUTA ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA/KUFUATA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUWA MAKINI
WANAPOTUMIA BARABARA HASA KWA KUTEMBEA PEMBEZONI MWA BARABARA NA KUVUKA
KATIKA SEHEMU ZENYE VIVUKO [ZEBRA CROSSING] ILI KUEPUKA AJALI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU WAKIWA NA NOTI BANDIA.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU 1. TIMOTH MGINA (27)
MKAZI WA SIMIKE – MBEYA 2. ALEX FUGAL (25) MKAZI WA MLOWO – MBOZI NA 3.
LUSEKELO STEVEN (20) MKAZI WA IWAMBI – MBEYA WAKIWA NA NOTI BANDIA 13
KILA MOJA IKIWA NA THAMANI YA SHILINGI 10,000/= SAWA NA SHILINGI
130,000/= ZENYE NAMBA BL-6882315 NOTI 3, BX 83652992 NOTI 7 NA BX 576441
NOTI 3. WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 04.03.2014 MAJIRA YA
SAA 18:13HRS JIONI HUKO KATIKA ENEO LA RUJEWA, KATA NA TARAFA YA RUJEWA
WILAYA YA MBARALI. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAENDELEA DHIDI YAO. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI NA MATUMIZI YA PESA HASA NOTI
ILI KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA JUU YA MTU/MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA
NOTI BANDIA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI
YAO ZICHUKULIWE.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA MAFUTA – DIESEL MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI.
No comments:
Post a Comment