Afisa ushirika mkoa wa Iringa John Kiteve akifungua mkutano huo |
Mwakilishi wa CRDB Iringa akifuatilia matukio katika mtandao huu |
Mwakilishi wa benk ya CRDB Iringa Bw Bruno akiwahamasisha kujiunga na bima mbali mbali |
………………………………………..
Na Francis Godwin Blog
WANACHAMA wa chama cha kuweka nakukopa cha Kilolo Teacher’s Sacco wilayani Kilolo mkoani Iringa wametakiwa kujenga uaminifu
katika kulipa madeni ya mikopo ambayo wamekopeshwa badala
ya kugeuza ni sadaka kwao.
Wito huo umetolewa na afisa ushirika wa mkoa wa Iringa John Kiteve wakati akifungua mkutano
mkuu wa mwaka leo mjini Kilolo.
Kiteve alisema kuwa wapo baadhi ya wanachama wasio
waaminifu ambao wamekuwa wakiomba mikopo na mara baada
ya kupewa mikopo hiyo wamekuwa wakishindwa kurejesha mikopo hiyo jambo ambalo linachangia vyama vingi vya ushiriki
na mikopo kuyumba hapa nchini.
“wapo baadhi ya wanachama ambao si waaminifu wamekuwa
wakichukua mikopo nawakati wakihama wamekuwa wakihama na madeni ya saccos bila kufika ofisini za Saccos na kueleza jinsi ambavyo atarejesha mikopo hiyo.
Hivyo aliwataka wanachama hao kujenga utamaduni wa kurejesha mikopo kwa wakati ikiwa ni pamoja na kutumia mikopo hiyo kwa maendeleo badala ya kutumia mikopo kwa anasa ambazo zitakwamisha urejeshaji wa madeni ya mikopo yao.
Pia Kiteve alisema kuwa Saccos hiyo ya walimu wilaya ya kilolo ni moja kati ya Saccos ambazo zimekuwa zikifanya vemana kuwa tofauti na saccos nyingine za walimu nchini kutokana na utaratibu mzuri wa Saccos hiyo kuwaunganisha walimu wa shule za msingi na sekondari.
Hata hivyo alisema ili kuondoa matabaka katika Saccos hiyo ni vema wanachama wote kuwa kitu kimoja badala ya kuwepo kwa matabaka kati
ya walimu wa shule za msingi na Sekondari jambo ambalo litaua nguvu ya Saccos hiyo.
katibu wa chama hicho Fabian Chavala alisema kuwa chama hicho kilianzishwa mwaka 2007 na kupata usajili wake IR 465 kikiwa na wanachama 60 wakiwemo wanaume 36 na wanawake 24ila kwa sasa kina wanachama 516 kati yao ni walimu wa shule za msingi ni 416 na wengine waliobaki ni kutoka shule za sekondari.
Hata hivyo alisema kumekuwepo na mafanikio makubwa katika chama hicho kwa chama kuongeza wanachama kwa kasi na kuwa na jengo lake pamoja na kuwa na mahusiano mazuri na taasisi za kifedha hasa benk ya CRDB
Mwenyekiti huyo alisema kuwa wanachama wa chama hicho wameendelea kunufaika na mikopo na kuwa hadi sasa wanachama 35 wamekopeshwa mikopo ya ununuzi wa vyombo vya usafiri yakiwemo magari manne na pikipiki 31,wanachama 343 wamepewa mikopo ya ujenzi wa nyumba za kisasa ,wanachama 156 wamekopeshwa mikopo ya masomo ya watoto wao na wanachama 28 wamepewa mikopo ya biashara na kilimo .

No comments:
Post a Comment