Hili
ni eneo la Ubungo ambapo Kumekuwa na kero kubwa ya wafanya bishara
wadogo wadogo kuegesha biashara zao za kila aina pembezoni mwa njia za
wapita kwa miguu jambo ambalo linasababisha usumbufu mkubwa kwa
watumiaji hao wa barabara hiyo.
Licha
ya usumbufu huo na kero hiyo, eneo hilo kutokana na msongamano wa watu
wengi sana, limekuwa ndio maskani kwa vibaka ambao hujipatia kipato
chao bila hata ya jasho kwa kujichanganya humo kama raia wa kawaida na
kufanya wizi.
Wakizungumza
watumiaji mbalimbali wa barabara hiyo wamelilalamikia Jiji na Manispaa
husika kwa kushindwa kuwataftia eneo husika wafanyabiashara hao wadogo
wadogo na kwamba kutokana na uzembe huo mkubwa wakuto wazuia nao
wameamua kuendelea kuleta kero
“Eneo
hili kwa kweli linatia Aibu sana kwa sababu hapa ndipo Lango kuu la
kuingia jijini na mara watu wanapo ingia wanakutana na kero hii ambayo
mimi binafsi naita ni uchafu, nasikitika sana kuona Jiji na Halmashari
husika wameshindwa kabisa kudhibiti na kuwataftia eneo husika hii ni
aibu”
Alizungumza mmoja wa watumiaji wa barabara hiyo ambaye hupita mara kwa mara.
Hizi ni Picha zilizopigwa moja kwa moja katika eneo hilo…
Wenye
kuuza Nguo za ndani katika eneo kama hili nao wapo ingawa napo kiafya
sio nzuri yaweza sababisha magonjwa ya ngozi kwa sababu watu wengi
wanaonunua huishia kuvaa moja kwa moja bila hata kufua
Eneo
hili lina vumbi na huku wakiwa wameanika T-Shirt zao na kuuza kitendo
kinacho sababisha kupatwa vumbi na kuhatarisha afya za watumiaji.
Hii
kali sana hawa Jamaa wanauza DVD kwa Tsh 500 hadi 1,000 bei ya juu sasa
swali linakuja hapa kuna kazi za Nje na ndani ya Tanzania Je Haki
miliki Mpo? na watu wa mapato hili mnalionaje?
Huu
ni uzibe wa Barabara kuu na wapita kwa miguu lakini vya kuzibia vimejaa
nguo mbalimbali je Hiyo ni sehemu halali ya kufanyia Biashara?
Katika eneo hili la Ubungo sio pembezoni mwa barabara pekee lakini hadi mabondeni biashara zinaendelea kwa kasi.
Hii
ndiyo hali Halisi ya eneo kutoka Ubungo Darajani karibia na mitambo ya
Gesi hadi eneo la watu wanaopandia magari ya kwenda Mwenge? Je
Halmashauri ya Jiji hamlioni hili? Je Manispaa husikia nanyie hamlioni
hili? Au hili ni eneo halali limepitishwa kwa ajili ya kufanya biashara
hizi?
Picha na Dar es salaam yetu
No comments:
Post a Comment