Mbunge wa jimbo la
Chalinze,Bagamoyo mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete wa kwanza kulia
alipoitembelea kituo cha afya cha Msoga juzi ,ambacho kinakaribia
kukamilika(Picha zote na Mwamvua Mwinyi)
Kituo cha afya cha Msoga,kata ya
Msoga ,Chalinze ,Bagamoyo Mmkoani Pwani,kikionekana kikiwa katika hatua
za mwisho kukamilika kwa ujenzi wake ulioanza mwaka jana,ambapo hadi
kukamilika kwake kitagharimu zaidi ya sh.mil 500
………………………………………………………………………………
KATIBU mkuu wa wizara ya afya na
ustawi wa jamii Donani Mmbando amesema serikali kupitia wizara ya afya
imejipanga kuhakikisha kunakuwepo na upatikanaji wa dawa,vifaa na vifaa
tiba kwa asilimia 100, ndani ya miaka mitatu ijayo.
Amesema endapo hakutakuwa na utekeleza wa suala hilo kwa kipindi alichokitaja watakuwa tayari kupimwa kwa hilo.
Mmbando ameyasema hayo jana,kijiji
cha Msoga,Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wakati alipoambatana
na ujumbe kutoka wizara hiyo kutembelea kituo cha afya cha Msoga
kujionea maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho unavyoendelea.
Ameeleza kuwa katika kutekeleza
mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN) ambapo sekta ya afya na ustawi wa
jamii inaingia rasmi eneo moja wapo la kipaombele ni upatikanaji wa dawa
,vifaa na vifaa tiba vya kutosha.
Aidha Mmbando amesema hatua
iliyopo sasa ni kuzungumza na wadau wa maendeleo wanaotaka kuwekeza
nchini kwa lengo la kujenga viwanda vya kuzalisha dawa kutokana na zaidi
ya asilimia 80 ya dawa hapa nchini zinaagizwa kutoka nje ya nchi kwa
gharama kubwa.
Amesema kuwa endapo kutakiwa na
kiwanda nchini kutawezesha nafasi ya ajira kwa wananchi,upatikanaji wa
dawa za kutosha ,gharama itakuwa nafuu ukilinganisha na gharama kubwa
inayotoza nje ya nchi na dawa zitapatikana kwa haraka.
Mmbando ameeleza kuwa anamini
katika kuandaa bajeti ya mwaka ujao wa fedha watahakikisha suala la
changamoto lililojitokeza la dawa litazingatiwa lisijitokeze tena kwa
wakati mwingine.
Hata hivyo amezitaka kamati maalum
katika ngazi zote nchini zinazosimamia uendeshaji wa huduma za afya
ikiwemo kamati za vituo,bodi za afya kuhakikisha zinasimamia na kupanga
uhitaji wa dawa za kuendesha vituo ,kusimamia na kudhibiti dawa
zinazopokelewa vituoni ili kuondokana na upotevu wa dawa unaotokea
njiani zinapokuwa zinasafirishwa kwenda vituoni.
Akizunguzmia suala la udhibiti wa
wizi wa dawa amesema kwasasa serikali kupitia bohari ya dawa waliamua
kuweka alama maalum kwenye vidonge na dawa zinazonunuliwa na serikali
hivyo zikikutwa katika maduka binafsi wataulizwa walipozitoa.
Mmbando ameeleza kuwa mkakati huo
utaendana na kuwataja wale watakaobainika kuiba dawa ili waaibike (name
and shame)ambapo watawatangaza kwenye vyombo vya habari na kuweka picha
ya mhusika kwa lengo la kupunguza vitendo hivyo .
Kuhusiana na kituo hicho ametoa
ushauri katika maeneo mbalimbali yanayohusiana na ujenzi kwani kituo
lazima izingatie miongozo na michoro inayotolewa na wizara ya afya na
ustawi wa jamii,na kuzingatia huduma zinazotolewa katika vituo hivyo
walibaini maeneo madogo yanayotakiwa kuboreshwa.
Nae
mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete pamoja na viongozi na
wasimamizi wa kituo hicho katika kata ya Msoga walipokea ushauri huo .
Ridhiwani amesema changamoto za kiafya katika kata hiyo na mahitaji ya kiafya bado ni makubwa hivyo ukamilishwaji wa kituo cha afya Msoga kitasaidia
kupunguza changamoto hizo hivyo aliitaka serikali kushirikiana nao pale
watakapohitaji msaada ili kukamilisha kituo hicho.
Ameeleza
kuwa kutokana na ajali nyingi zinazotokea mara kwa mara katika barabara
ya Chalinze-Segera kituo cha afya Msoga kitawezesha kupunguza mzigo wa
vituo vya afya vya Lugoba,Chalinze na Lugoba ambavyo vimekuwa vikipokea
majeruhi wengi wa ajali .
Kituo
cha kisasa cha afya cha Msoga,kilianza ujenzi wake mwaka 2013 na
kinatarajiwa kukamilika mwaka ujao na hadi kukamilika kwake kitagharimu
kiasi cha sh mil.500.
No comments:
Post a Comment