Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
HATIMAYE
 `Deal Done`!!. Wekundu wa Msimbazi Simba Sc, Taifa Kubwa wamehalalisha 
kuondoka kwa kipa wake Mganda, Abel Dhaira baada ya leo hii kumsajili 
mlinda mlango wa zamani wa Dar Young Africans, raia wa Ghana, Yaw Berko 
kwa mkataba wa miezi 6.
Berko
 ametua leo jijini Dar es salaam  na pipa akitokea kwao Ghana, 
(Magharibi mwa Afrika) na amekuja kufanya kazi na kocha mpya wa klabu ya
 Simba,  Mserbia Zdravko Lugarusic ambaye pia  mchana wa leo amesaini 
mkataba wa miaka miwili kurithi mikoba ya kocha, Abdallah Athuman Seif 
`King Kibadeni Mputa` aliyabebeshwa virago kwa madai ya kushindwa 
kufanya vizuri mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Kusajili
 wa kwa Berko kumekalimisha safari ya Dhaira kufanya kazi Msimbazi kwani
 tayari uongozi wa klabu hiyo ulishaondoa imani juu ya kipa huyo wakidai
 kiwango chake hakiridhishi,  kwani amekuwa akifungwa mabao mepesi sana.
Vita
 kama kawa:  Berko kamwaga wino leo Msimbazi, mpinzani wake wa wakati 
ule akiwa Yanga, Juma Kaseja amejiunga na wanajangwani dirisha dogo la 
usajili, kutokana na ubora wa makipa hawa wawili, upinzani mkali 
unategemewa
Kipa
 huyo aliwadakia watani wa jadi wa Simba, Dar Young Africans tangu mwaka
 2010 baada ya kujiunga katika dirisha dogo mnamo desemba mwaka 2009 
akitokea kufanya kazi na klabu ya Ghana ya Liberty Proffessionals .
Berko
 alifanya kazi na Yanga  hadi msimu uliopita alipotolewa kwa mkopo 
kwenda kufanya kazi yake katika klabu ya FC Lupopo ya DRC Kongo.
Baada
 ya kufika mjini Lubumbashi, Berko alizingua kufanya kazi na kuamua 
kurejea jijini Dar es salaam kujiunga na Yanga kwa madai ya 
kutoridhishwa na hali ya klabu hiyo , lakini uongozi ulimtupilia mbali 
kwa kuuvunja mkataba wake na kumlipa `Mtonyo` wake  kwani tayari wakati 
huo walikuwa wameshapata kipya mpya Ally Mustapha ` Bartez` aliyetokea 
Simba na Berko akapaa angani kurejea kwao Ghana.
Tanzania One: Mlinda Mlango mpya wa Yanga, Juma Kaseja ataendelea kupambana na kipa mwenzake bora, Yaw Berko wa Simba.
Wakati
 Berko akiidakia Yanga, mpinzani wake langoni alikuwa kipa wa zamani wa 
Wekundu wa Msimbazi Simba sc, Juma Kaseja ambaye aliachwa na Simba msimu
 uliopita, lakini upinzani unaendelea tena baada ya Kaseja `Tanzania 
One` kujiunga na Yanga na leo hii ameanza mazoezi katika uwanja wa Bora 
kijitonyama, jijini Dar es salaam.
Kusajiliwa
 kwa Kaseja Yanga, kumemkutanisha tena na makipa wenzake wawili aliowahi
 kuwakalisha benchi kwa muda wote wakiwa Simba, Ally Mustapha `Bartez` 
na Deogratius Munish `Dida`.
Tusubiri maamuzi ya benchi la ufundi la Yanga chini ya kocha Mholanzi, Ernie Brandts kuamua ni kipa gani atakuwa chagua lake.
Leo
 hii katika mazoezi ya Yanga, makipa hao Bartez na Kaseja walikuwa 
kivutio walipokuwa wakifanya mazoezi pamoja chini ya kocha wa Makipa, 
Mkenya Razack Ssiwa


No comments:
Post a Comment