WILAYA YA MOMBA – MAUAJI. 
MNAMO
 TAREHE 01/12/2013 MAJIRA SAA 01:00HRS HUKO MAENEO YA SIKANYIKA KATA YA 
TUNDUMA TARAFA YA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA, MTU MMOJA 
ALIYETAMBULIKA KWA JINA MOJA LA SIMBEE S/O ?, ANAYEKADIRIWA NA KUWA NA 
MIAKA 46-50, MKAZI WA MAPOROMOKO ALIUAWA  NA MWENZAKE MENSON S/O 
MWAZEMBE, MIAKA 58, MNYIHA NA MKAZI WA MAPOROMOKO, KUJERUHIWA NA KULAZWA
 KATIKA ZAHANATI YA TUNDUMA KWA MATIBABU BAADA YA  KUPIGA MARUNGU/FIMBO 
SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO NA  MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. MBINU 
ILYOTUMIKA NI KUWAVAMIA WAKIWA LINDONI NA KUWAFUNGA KAMBA KISHA 
KUWASHAMBULIA, CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO HAKIJAFAHAMIKA. KAIMU KAMANDA
 WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI  
ANATOA  WITO/RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI WALIPO 
WATUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE 
MKONDO WAKE, VINGINEVYO WAJISALIMISHE WENYEWE.
WILAYA YA RUNGWE – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
NA KUSABABISHA KIFO.
NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
 TAREHE 30/11/2013 MAJIRA YA SAA 19:00 HRS HUKO KATUMBA  KATA YA  
KATUMBA TARAFA YA  TUKUYU WILAYA YA  RUNGWE MKOA WA MBEYA. GARI 
LISILOFAHAMIKA NAMBA ZA USAJILI WALA DEREVA AINA NA FUSO LILIMGONGA 
MTEMBEA KWA MIGUUU AITWAYE YESAYA S/O MWENDESI, MIAKA 56, MNYAKYUSA, 
MKAZI WA KATUMBA NA KUSAFARIKI AKIWA ANAPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI
 YA SERIKALI MAKANDANA TUKUYU. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA DEREVA 
ALIIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO.  KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA 
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI  WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA 
WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA USAFIRI KWA 
KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA BARABARANI HASWA KATIKA KIPINDI HIKI CHA 
KUELEKEA MWISHO WA MWAKA 2013 ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.  
AIDHA ANATOA RAIA KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO 
MTUHUMIWA HUYO AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA 
ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA
WILAYA YA KYELA – AJALI YA GARI KUGONGA MTI NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
 TAREHE 30/11/2013 MAJIRA YA SAA 13:30HRS HUKO KIJIJI CHA BUGESI KATA 
YA   KAJUNYUMELE TARAFA YA  UNYAKYUSA WILAYA YA  MKOA WA MBEYA, GARI NO 
T.896 BBG AINA YA  COROLA LIKIENDESHWA NA DEREVA ANTONY S/O MALILI, 
MIAKA 31, MNYAKYUSA, MKAZI WA KAJUNYUMELE LILIGONGA MTI NA KUSABABISHA 
KIFO CHA VICTORIA D/O MALILI, MIAKA 49, MNYAKYUSA, MKULIMA NA MKAZI WA 
KAJUNYUMELE NA MAJEREHA KWA ABIRIA MMOJA PAMOJA NA DEREVA. MAJERUHI 
WAMELAZWA KATIKA HOPITALI YA WILAYA YA  KYELA NA MWILI WA MAREHEMU 
UMEHIFADHIWA HASPITALINI HAPO, CHANZO CHA AJALI NI  MWENDO KASI. 
KAIMUKAMANDA WA P OLISI MKOA WAMBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI 
BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUUMIAJI WENGINE WA 
BARABARA KUWA MAKINI NA MATUMIZI BORA YA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI 
HASWA WAKATI HUU KUNAPOELEKEA KUUKARIBISHA 2014 NA KUAGA MWAKA 2013. TUSISHABIKIE MWENDO KASI KWANI AJALI NI NOMA.
 [B.N.MASAKI  – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:
Post a Comment