Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib 
Bilal,  akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mpango wa Taifa wa 
Kudhibiti Ukimwai, chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. 
Angela Ramadhan, wakati alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonyesho 
katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, yaliyofanyika kwenye 
Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Kaimu Mkuu
 wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantum Mahiza, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume 
ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dkt. Fatma Mrisho. Picha na OMR 
  
  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akifurahi
 na mtoto Samir Isagetee (miezi 7) akiwa na Mama yake, Lilian Amani, 
wakati  alipotembelea katika Banda la Watu wanaoishi na Virusi vya 
Ukimwi NACOPHA, katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, 
zilizofanyika leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. 
Mtoto huyo ni mmoja kati ya watoto waliozaliwa na wazazi wenye 
maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na yeye kuzaliwa salama. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea mabanda katika maadhimisho hayo. 
 
 
 
 
Baadhi ya wanafunzi wakipita na mabango yenye ujumbe mbalimbali mbele ya  Jukwaa
 Kuu, wakati Makamu alipokuwa akipokea maandamano hayo kwenye  
maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, 
jijini Dar es  Salaam, leo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akihutubia
 wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, kwenye 
Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo. 
Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib 
Bilal, akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Mpango Mkakati wa 3 wa 
Kitaifa wa Kudhibiti Ukimwi (NMSF3), wakati wa sherehe za Maadhimisho ya
 Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja 
jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa 
Jamii, Dkt. Seif Rashid, (wa pili kulia) ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es
 Salaam, Mwantum Mahiza, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi
 Tanzania, Dkt. Fatma Mrisho.  
 
 
Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
 akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi.  Picha Zote na OMR
 


No comments:
Post a Comment