TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, December 3, 2013

Rais Kikwete aonya siasa kwenye kilimo

Rais Kikwete akihutubia kijiji cha Rulenge 
Rais Jakaya Kikwete, ameaonya wanasiasa nchini kuingiza mambo ya siasa kwenye kilimo, hasa kilimo cha mkataba kwa wakulima.
Alitoa onyo juzi mjini Nyashimo, wilayani Busega, katika siku yake ya mwisho ya ziara ya siku tano katika Mkoa mpya wa Simiyu.
Rais Kikwete alisema kuna baadhi ya wanasiasa, wamekuwa wakiyatumia majukwaa kupotosha ukweli juu ya manufaa ya kilimo cha mkutaba kwa mkulima, badala ya kuwaelimisha, nini manufaa ya kilimo hicho.
Akiwahutubia mamia ya wakazi wa mji mdogo wa Nyashimo, Rais Kikwete alisema wanasiasa hao hawana tofauti na wakoloni, ambao mikataba yao ilikuwa ni za kumkomoa mzalendo, kwa mikataba isiyo na tija kwa mwananchi.
Alionya kuwa kamwe wanasiasa wasipambane na kilimo hicho, kwa sababu ya manufaa yao binafsi ya kisiasa na badala yake waangalie ni kwa namna gani atanufaika na kilimo cha mkataba.
Badala yake, Rais Kikwete aliwataka wanasiasa na viongozi wote kutoa elimu kwa wakulima juu ya manufaa ya kilimo cha mkataba kinacholenga kuwakomboa.
Akizungumzia ruzuku ya mbegu ya pamba, Rais alionyesha kusikitishwa kwake ni jinsi gani ruzuku hiyo imeoendolewa, na kuahidi kutafuta mwarobaini wa kilio cha wakulima wa zao la pamba wakiwamo wa mkoa wa Simiyu.
“Ile ruzuku ya mbegu ya pamba mbona imeondoka, nitawauliza wahusika…niachieni mimi na majibu yake mtayapata msimu unaofuta,” alisema.
Kuhusu mbegu za pamba ya manyonya na isiyo na manyoya, Rais Kikwete alisema wataalam na viongozi katika maeneo yao, hawanabudi kuwaeilimisha wakulima manufaa ya kupanda mbegu bora yenye uzalishaji wenye tija.
Kuhusu wafugaji, aliwataka wanasiasa kuacha kushabikia ufugaji wa kuhamahama na kueleza kuwa kamwe serikali haitawavumilia hasa wenye tabia ya kuvamia maeneo ya wakulima na kusababisha uharibifu wa mazingira.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment