Na Frank Mvungi
 Taasisi yaTiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) imepanga kutumia zaidi ya Bilioni 17 katika ujenzi wa awamu ya Tatu ya Mradi wa Taasisi yaTiba ya Mifupa   na Mishipa ya Fahamu (MOI phase 111) hadi mradi huo utakapokamilika mapema mwakani.
 Hayo
 yamesemwa leo na Meneja Uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Jumaa Almasi 
wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
 Almasi
 alisema kuwa Ujenzi wa jengo hilo jipya lenye ghorofa 7 ambao 
unaendelea ukikamilika utaongeza maeneo ya kutolea huduma,Vitanda 
vitafikia 380 kutoka 159 vilivyopo sasa hali ambayo itapanua wigo wa 
huduma zinazotolewa kwa sasa.
 “Mradi
 huu utasaidia kuongeza ufanisi na huduma zinazotolewa na taasisi kwani 
ukikamilika utaongeza maeneo ya kutolea huduma kwa kupunguza msongamano 
wa wagonjwa mawodini kutokana na kuongezeka kwa vitanda kutoka 159 hadi kufikia 380” Alisema Almasi.
 Aliongeza
 kuwa huduma nyingine zitakazotolewa  ni CT SCAN,MRI,huduma za Cybernife
 na Digital Antiograph ambazo kwa Sasa hazitolewi katika Taasi  hiyo .
 Alibainisha
 kuwa MOI ni moja ya Taasisi  zenye vifaa bora vya upasuaji pamoja na 
vyumba vya upasuaji vinavyokikidhi viwango vya kimataifa kusini mwa 
jangwa la Sahara baada ya Afrika ya kusini.
 Alisema
 kuwa hali hiyo ni matokeo ya juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali 
katika kuboresha huduma za afya nchini ambapo wameweza kupatiwa vifaa 
vya kisasa pamoja na wataalamu waliobobea katika  huduma za tiba ya 
mishipa ya fahamu na upasuaji wa uti wa mgongo.
 Bw.
 Almasi  alibainisha kuwaTaasisi ya MOI imeendelea kushirikiana na 
Taasisi za Kimataifa  zinazotoa huduma za afya kama SIGN GROUP  ya  
nchini Marekani  ambayo imekuwa ikitoa msaada wa vifaa tiba ikiwa ni 
alama ya ushirikano mzuri uliopo kati ya Taasisi hiyo na mashirika ya 
Kimataifa.


No comments:
Post a Comment