Aliyekuwa
 Miss Tanzania 1999, ambaye pia ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano 
wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania , Hoyce Temu akipozi mara baada ya 
kulamba Nondozzz ya shahada ya Uzamili wa Mawasiliano ya Umma katika 
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine jijini Mwanza.
Hoyce Temu akipata Ukodak na Mdau wa tasnia ya habari nchini.
Hoyce Temu katika pozi na marafiki zake mara baada ya kulamba Nondozz.
Pongezi
 pia ziende kwa Dada Lulu Musa Afisa Uhusiano wa Ofisi ya Makamu wa Rais
 Mazingira kwa kulamba Nondozz ya shahada ya Uzamili wa Mawasiliano ya 
Umma katika chuo cha St. Augustine University kwenye mahafali ya 15 ya 
chuo hicho yaliyofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa Juma.
Mbali
 na kula Nondozz kwenye siku hiyo maalum Hoyce Temu ambaye pia ni 
Mtangazaji wa Kipindi cha Mimi na Tanzania aliamua kufanya mahojiano na 
baadhi ya wahitimu kwa ajili ya kipindi chake.
Mlimbwende
 Hoyce Temu akizungumza na mwandishi wa habari wa ITV kuhusiana na 
taalum aliyoipata itakavyoweza kuboresha utendaji wake kazini pamoja na 
kuendelea kuisaidia jamii inayomzunguka kupitia kipindi chake cha Mimi 
na Tanzania.
Mwandishi wa habari wa kituo cha ITV,  Shaban Tole akimpongeza Hoyce Temu.
Hoyce Temu katika picha ya kumbukumbu na marafiki.
Hoyce Temu akiondoka eneo la tukio na furaha isiyo na kifani.








No comments:
Post a Comment