TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, December 5, 2013

TANZANIAONE , STAMICO KUSHIRIKIANA

badilishana 
Na Kiza Sungura- MAELEZO_Dar es salaam
Shirika la Madini la Taifa [STAMICO] limeingia mkataba wa ubia na Kampuni ya TanzaniteOne Mining Limited [Tanzanite One] kuhusu uchimbaji wa pamoja wa madini, ya Tanzanite katika kitalu C, Mirerani.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO Gray Mwakalukwa wakati akitoa ufafanuzi kwa  waandishi wa habari mara baada ya hafla fupi ya kusaini mkataba huo.
Mwakalukwa alisema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini kutoa leseni ambayo inawawezesha STAMICO  kumiliki asilimia 50 na TanzaniaOne watabaki na  asilimia 50.
Alisema kuwa umiliki huo unatokana na Serikali kusimamia utekelezaji wa Sera ya Madini ya mwaka 2009 na Sheria ya Madini ya mwaka 2010 ambapo chini ya sharia hiyo, Kampuni za kigeni haziruhusiwi kumiliki hisa zaidi ya asilimia 50 katika uchimbaaji wa vito.
Mwakalukwa aliongeza kuwa mkataba huo umezingatia makubaliano ya awali yaliyotiwa saini mapema mwaka huu ambayo yataka STAMICO na Tanzanite One kuwa  na gawio sawa la asilimia 50 kwa hamsini litakalotokana na faida.  
Alitaja baadhi ya mambo waliokubaliana ni pamoja na mitambo ya uchimbaji na uzalishaji itabaki kuwa ni mali ya Tanzanite One itaendelea  kutumika na wabia wataifanyia matengenezo itakapoharibika.
Mwakalukwa alisema kuwa jambo jingine waliokubaliana ni pamoja na kuanzisha kitengo maalum cha ufuatiliaji na tathmini ya shughuli zote za mgodi kitakachoundwa kutoka kwa wajumbe wa kila pande.
Naye Mwenyekiti wa Tanzanite One, Balozi  Ami Mpungwe alisema kuwa hatua ya Kampuni yake kusaini  mkataba huo ni sehemu ya  kutekeleza sera ya uchimbaji  wa madini nchini na ni  hatua nzuri  ya  kuhakikisha ulinzi na usalama madini ya Tanzanite. 

No comments:

Post a Comment