![]()  | 
| Mwakilishi wa Mitandao ya Kijamii nchini (CCT), Jennifa Chiwute | 
Watoto
 yatima nchini  wako hatarini  kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia
 ilikinganishwa na kundi la wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.
Akizungumza
 jana katika  mdahalo  ulioandaliwa na mtandao wa kupinga ukatili wa 
kijinsia (MKUKI) ulioratibiwa na  Shirika la Kupinga Ukatili wa Kijinsia
 Tanzania (AFNET)Kanda ya Kati uliofanyika mjini hapa, Mwakilishi wa 
Mitandao ya Kijamii nchini (CCT), Jennifa Chiwute, alisema  taarifa ya  
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa mwaka 2009 
kuhusiana na vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini,  imeonyesha kundi 
hilo la watoto yatima liko kwenye hatari zaidi ya kufanyiwa vitendo 
hivyo kwa kuwa wengi wao hawana ulinzi kutoka kwa mtu yeyote.
Akiwasilisha
 mada kuhusiana na mpango wa kukomesha vitendo hivyo, Chiwute,  alisema 
taarifa hiyo ilionyesha kuwa asilimia 30 ya wasichana na asilimia 14.3 
ya wavulana,  waliwahi kutendewa kitendo kimoja cha ukatili wa kijinsia 
kabla ya kufikisha umri wa miaka 18 huku asilimia 60 ya wasichana 
walilazimishwa kujamiina.
Alibainisha 
 pia inaonyesha kuwa wasichana hao walilazimishwa kujamiiana na ndugu,  
jirani, marafiki na watu wasiowafahamu wenye umri mkubwa.
“Waathirika
 wenyewe wanafanyiwa kwenye maeneo ya nyumbani kwa mtu, shuleni au 
njiani wakati wa kwenda au wa kurudi shuleni,” alisema Chiwute.
Alisema vitendo hivyo ni pamoja na ukatili wa kipigo, ukeketaji, kingono na kiakili.
Alisema vitendo hivyo ni pamoja na ukatili wa kipigo, ukeketaji, kingono na kiakili.
Alionya
 kuwa iwapo vyombo vya dola havitachukua hatua za kisheria kwa 
wanaotenda vitendo hivyo, hali itazidi kuwa mbaya zaidi kwa siku zijazo.
“Vyombo
 vya serikali vimeshindwa kusimamia kwa dhati utekelezaji wa sheria 
zinazolinda haki za wanawake, watoto na watu wenye ulemavu kwa sababu ya
 rushwa,”alisema Chiwute.
Kwa 
upande wake, Mkurugenzi wa  AFNET Tanzania,  Sarah Mwaga, alisema ni 
wajibu wa wadau wote na watetezi wa haki za binadamu kuungana kukomesha 
vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vina madhara makubwa kwa 
watendewa.
Naye 
Mkuu wa Kitengo cha Dawati la Jinsia Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, 
Hamida Hiki, alisema kuwa jeshi hilo linakabiliwa na changamoto ya jamii
 kuwa na mfumo dume ambao ndiyo chanzo cha vitendo vya ukatili ambavyo 
vinasababisha wimbi la watoto wa mazingira hatarishi mitaani.

No comments:
Post a Comment