
Wapiganaji
 wa Boko Haram wameshambulia ngome ya kikosi cha anga cha Jeshi 
Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na kuharibu helkopta mbili maafisa wa 
serikali wamesema.
Mashuhuda
 wa tukio hilo wanasema mamia ya wapiganaji wameshambulia maeneo kadhaa 
katika mji wa Maiduguri kuanzia mapema asubuhi siku ya jumatatu.
Amri 
ya kutotembea ovyo ya saa 24 imetangazwa katika jimbo la Maiduguri. Na 
uwanja wa ndege unaotumiwa na wananchi umefungwa kwa muda.
Mwandishi
 wa habari wa BBC anasema shambulio hilo lililopangwa ni shambulio kubwa
 ambalo limerudisha nyumba juhudi za Jeshi la Nigeria.
Maelfu
 ya watu wameuwawa nchini Nigeria na wapiganaji hao tangu mwaka 2009 
wakati Boko Haram walipoanza mashambulizi ya kutaka kusimika utawala 
unaoegemea sharia ya kiislamu.
CHANZO: BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment