TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, December 5, 2013

Lukuvi Kuwa Mgeni Tamasha la Krismasi Dar es Salaam.

William Lukuvi 
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Krismasi Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Desemba 25 mwaka huu.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa maandalizi kuhusiana na tamasha hilo yanaenda vizuri.
“Hamasa imekuwa kubwa pengine kuliko matamasha mengine ambayo Kampuni yangu ya Msama Promotions imewahi kuyaandaa. Waimbaji wanatamani siku ifike wafanye mambo, mashabiki nao wanatamani siku ifike waone mambo.
“Pia nafurahi kuwajulisha kuwa Waziri Lukuvi amekubali kuwa mgeni rasmi Desemba 25 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, naamini siku hiyo itakuwa burudani ya aina yake. Namshukuru sana kwa kuungana nasi,” alisema Msama, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Tamasha la Pasaka.
Alisema kiingilio cha chini katika tamasha hilo kwa upande wa Uwanja wa Taifa kitakuwa sh. 5000 na viingilio vingine vitakuwa sh 10,000 na sh.20,000 kwa majukwaa maalum A na B.
“Pia watoto watachangia sh. 2,000, tumeweka viingilio vya kawaida ili wote tuweze kuhudhuria Uwanja wa Taifa,” alisema Msama na kuongeza kuwa kwa mikoani viingilio ni sh 5,000 kwa wakubwa na watoto itakuwa Sh 2,000.
Waandaaji hao wamepanga tamasha hilo lifanyike Desemba 25 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na siku inayofuata Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, kisha Desemba 28 Uwanja wa Mkwakwani Tanga na Desemba 29 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

No comments:

Post a Comment