Washabiki
 watakaoshuhudia mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wasichana wenye 
umri chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Tanzanite) na Afrika Kusini 
watalipa kiingilio cha sh. 1,000.
Mechi
 hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano hiyo itachezwa Jumamosi 
(Desemba 7 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 
kamili jioni.
Kiingilio
 cha sh. 1,000 ni kwa viti vya rangi ya kijani, bluu na orange. 
Viingilio vingine kwa mechi hiyo vitakuwa sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000
 kwa VIP B wakati VIP A watalipa sh. 10,000.
Tanzanite
 chini ya Kocha Rogasian Kaijage inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa 
Kumbukumbu ya Karume na ule wa Taifa kujiandaa kwa mechi hiyo. Kambi ya 
Tanzanite hivi sasa imehamia Msimbazi Hotel kutoka Ruvu mkoani Pwani.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments:
Post a Comment