Naibu
 Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Bi. Salama Abuud Talib akimkaribisha Makamu
 Mwenyekiti UWT Bi. Asha Bakari Makame kuzungumza na wandishi wa Habari 
kuhusu miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wa Jumuiya hiyo. 
 
 
Makamu
 Mwenyekiti UWT Bi. Asha Bakari Makame akizunguza na wandishi wa Habari 
kuhusu miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui 
Mjini Zanzibar. 
 
 
Makamu
 Mwenyekiti UWT Bi. Asha Bakari Makame akisisitiza kitu alipokuwa 
akizungumza na wandishi wa Habari kuhusu miaka 50 ya Mapinduzi ya 
Zanzibar ofisini Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini 
Zanzibar.
Zanzibar.
Mwandishi
 wa Habari wa Chuchu Fm Radio Rahama Suleiman akitaka ufafanuzi wa kitu 
kwenye Mkutano wa UWT ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar. 
(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Na Ali Issa Maelezo-Zanzibar
Umoja
 wa wanawake wa CCM Tanzania (UWT) umesema vikundi vingi vya ushirika 
vya kina mama vimesaidiwa  fedha nyingi za mikopo kujiendesha lakini 
inaonekana bado kuna baadhi ya kinamama wanashindwa kuviendesha vikundi 
hivyo kutokana na kutokuwa na dira nzuri kuviendeleza vikundi hivyo.
Hayo
 yamesemwa leo huko ofisi kuu ya Chama cha Mapinduzi Kisiwandui Mjini 
Zanzibar na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Salama Aboud Talib wakati 
alipokuwa na mazungumzo na waandishi wa Habari katika kuadhimisha 
sherehe za miaka 50 ya mapinduzi Zanzibar kwa Jumuiya ya wanawake wa CCM
 Zanzibar.
Amesema
 umoja wa wanawake Tanzania  kupitia wake wa viongozi wa kuu wa Serikali
 na tasisi nyengine wametoa  pesa nyingi katika kusaidia vikundi vya 
kinamama ili kujikwamua na umasini na kuviendeleza vikundi vyao kupata 
tija jambo ambalo baadhi ya viongozi  wa vikundi hivyo hushindwa 
kuviendeleza na hatimae kutofikia malengo ya kuazishwa kwake.
Amesema
 hali hiyo si njema kwani inarudisha nyuma juhudi za viongozi jambo 
ambalo lengo la chama cha Mapinduzi ni kuijenga jamii ya wanawake kua na
 muelekeo mzuri kimaendeleo na kujinasua na umasikini.
“Wake
 waviongozi wetu huwapa pesa nyingi wana vikundi  kuwasaidia wanawake 
  lakini vikundi hivyo hushindwa kuziendeleza pesa zile na baadae 
kikundi huwa kina shindwa kujiendeshana pesa kupotea,” alisema Salama.
Aidha
 alifahamisha kuwa wanashindwa kufahamu kupotea kwa pesa hizo kwani 
amesema kabla ya kutolewa peasa hizo vikundi hupatiwa mafunzo kutoka kwa
 wataalamu ili waweze kuviendesha.
Bi.Salama
 alisema hali hiyo haifurahishi hata kidogo kuona pesa zinapotea na 
vikundi kufa na italazimika kwa wanavikundi kutafuta mbinu mbadala 
badala ya zile za kitalamu ili kuona vikundi vina piga hatukubwa za 
kimaendeleo.
Nae
 Makamo mwenyekiti UWT Bi. Asha Bakari Makame alisikitishwa sana na 
suala la unyanyasaji kwa watoto na wanawake na kuishauri Serikali 
iangalie kwa umakini suala hilo kwani inaonekana kuna mtandao mkubwa wa 
kuwadhalilisha watoto kwa kuwanajisi hali ambayo ni hatari katika taifa 
hili la Zanzibar.
Amesema
 Serikali iangalie sheria zake na kuzifanyia marekebisho kwani watoto 
wanaharibiwa vibaya na watuhumiwa kushindwa kuingia hatiani jambo ambalo
 sisahihi kwa watoto kudhalilishwa kwa kunajiwa na kutengwa na 
wazaziwao.  
Makamo
 huyo alisifu juhudi za Jumuiya hiyo inazochukua kwa kua karibu na wana 
nchi kupitia Serikali kuu kwa kufuata ilani ya chama cha Mapinduzi.
Alisema
 hivi sasa wanawake wa Zanzibar wamefaidika sana na Jumuiya hiyo kwa 
kupata frusa katika ngazi za Sekikali na kuweza pia kupata elimu na 
ajira kwa idadi ya wanawake ambayo ni wazi kuwa wanwake wa Zanibar 
wanathaminiwa sana na serikali yao.
Bi.Asha
 Bakari alizipongeza Serikali zilizo pita,Viongozi wa Afroshirazi na hii
 ilioko madarakani kwa kuyaendeleza Mapinduzi matukufu yalio mkomboa 
mwanamke kutoka katika utwala wakisultani na 1964 kua Taifa  huru,lenye 
 Umoja amani na mshikamano.

No comments:
Post a Comment