TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, December 3, 2013

Serikali yatia saini mikataba yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni Tsh.538 ujenzi wa barabara

Pix 01Wakandarasi na Washauri wakiwa wanamsikiliza kwa makini Mtendaji Mkuu wa TANROADS mhandisi Patrick Mfugale (hayupo pichani). Pix 02Mameneja wa TANROADS toka Mikoa mbalimbali ya Tanzania wakiwa wamehudhuria sherehe za kuweka saini mikataba hiyo.
Pix 03 
Baadhi ya wabunge wanaotoka katika mikoa ambayo miradi hiyo ya ujenzi wa barabara itafanyika wakishuhudia sherehe za kutia saini mikataba ya ujenzi wa barabara hizo mapema hii leo jijini Dar  Pix 04 
Mwakilishi toka Benki ya Maendeleo ya Afrika bwana Patrick Musa akielezea mipango ya Benki hiyo kuendelea kutoa mikopo katika maradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Pix 05 
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) Bwana Onishi Yasunori akieleza mikakati ya shirika hilo kutoa mikopo katika shughuli mbalimbali za maendeleo hapa nchini huku akionesha moja ya ramani ya ujenzi wanaotarajia kufanya hapa nchini.
Pix 06 
Waziri wa Ujenzi Dkt John Magufuli akisistiza jambo kwa waandishi wa wakandarasi mapema hii leo jijini Dar es Salaam, wakati wa utiaji saini mikataba mitatu ya ujenzi wa barabara. pix 07 
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale (wa pili kulia) akiweka saini Mkataba ujenzi wa barabara ya Mayamaya hadi Mela, wa pili kulia ni mwakilishi wa Kampuni ya china Henan International Cooperation Group Co. Ltd. Bwana Ghuo Zhijian, kulia ni  Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) Bwana Onishi Yasunori  na kushoto ni Mwakilishi toka Benki ya Maendeleo ya Afrika bwana Patrick Musa.
Picha Zote na Eliphace Marwa – MAELEZO
Na Eliphace Marwa (Maelezo)
Serikali  imetia saini mikataba mitatu  ya ujenzi wa barabara yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni Tsh.538  za Kitanzania  kwa ushirikiano toka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) mapema hii
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za kutia saini mikataba hiyo,Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrck Mfugale alisema  kati ya fedha hizo ADB wanachagia asilimia 65.80 , JICA  asilimia 29.2 ambazo wametoa mkopo  na Serikali inachangia asilimia tano.
“Mikataba iliyotiliwa saini hii leo ni pamoja na ujenzi wa sehemu ya Mayamaya hadi Mela yenye urefu wa kilomita 99.35 inayojengwa na Kampuni ya China Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO) kwa gharama ya zaidi bilioni mia moja kwa muda wa miezi thelasini na sita,” alisema Mfugale.
 Alizitaja  barabara nyingine ni  Mela hadi Bonga  yenye urefu wa kilomita 88.8 inayojengwa na Kampuni ya China Railway  Seventh Group  kwa gharama ya zaidi Sh. bilioni 88 , ambapo  muda wa utekelezaji ni miezi thelasini na sita.
Mkataba wa mwisho ni wa ujenzi wa barabara ya Mangaka hadi Mtambaswala yenye urefu wa kilomita 65.5 itakayojengwa na Kampuni  ya Sichuan Road and Bridge (Group) Corporation kwa gharama ya zaidi ya Sh.bilioni 59 na muda wa utekelezaji ni miezi ishirini na nne.
 “Napenda kuwapongeza Benki ya Maendeleo ya Afrika pamoja na Shirika la Maendeleo la Japan kwa ushirikiano wao kwani sio mara ya kwanza kutupatia mkopo kwa ajili ya ujenzi wa barabara zetu na tunaahidi kuzisimamia ili ziwe katika ubora unaotakiwa”, alisema Mfugale.
Aidha naye Waziri mwenye dhamana ya ujenzi Dkt. John Magufuli alishukuru ADB  na JICA kwa mkopo huo na kutoa angalizo kwa wakandarasi wasio makini na kazi zao kukaa chonjo kwani sasa hakuna huruma kwao tena.
“Napenda kuwatahadharisha nyie makandarasi mlioko hapa kama kuna yeyote kati yenu hataweza kufanya kazi kwa ubora na wakati basi asisaini mkataba huu”, alisema Dkt Magufuli.
Nao wawakilishi toka ADB na JICA  walimshukuru Waziri Magufuli kwa usimamizi imara wa miradi mbalimbali ujenzi inayoendelea kote nchini.
Hii  si mara ya kwanza kwa ADB  na JICA  kutoa mkopo kwa ajili ya ujenzi wa barabara  kwani  Machi mwaka , 2010 walitoa mkopo kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Iringa mpaka Dodoma yenye urefu wa kilomita 260 na barabara ya  Namtumbo mpaka Tunduru yenye urefu wa kilomita 193.

No comments:

Post a Comment