Wamiliki
 wa uwanja wa kumbukumbu ya sokoine jijini Mbeya wameanza rasmi mchakato
 wa kufanyia marekebisho uwanja huo kama walivyoagizwa na shirikisho la 
soka Tanzania TFF.
Meneja
 wa uwanja huo, Modestus Mbande Mwaluka amesema ndani ya wiki mbili 
watakuwa wamekamilisha marekebisho na baada ya hapo wataanza kumwagilia 
maji sehemu ya pichi.
“Jana
 tumeanza kwa kung`oa magoli, leo tunaanza kushughulikia sehemu ya ndani
 ya uwanja, magreda yameshaagizwa na lazima yaje ili kuutifua na kupanda
 nyasi mpya. Kizuri pesa ipo ndugu yangu”. Alisema Mwaluka.
“Kizuri
 zaidi hiki ni kipindi cha mvua jijini hapa, itasaidia sana ukizingatia 
uwepo wa maji ya bomba. Nyasi zitakua haraka na kubadili mandhari ya 
uwanja huu”. 
Mwaluka
 amesema wanataka uwanja huo uwe mzuri na utumike katika michuano ya 
kimataifa, na kwasasa watarekebisha miundo mbinu yote ikiwemo vyumba vya
 kubadilishia nguo kwa wachezaji, vyoo na maeneo mengine muhimu.
“Ujue
 tulishasema kutoka mwanzo kuwa, tupo katika mkakati madhubuti wa 
kuufanya uwanja wetu uwe bora, tulianza na uzio, tumeshaimarisha, sasa 
tunafuata sehemu ya ndani `Pitch`, tutafuata vyumba vya kubadilishia 
nguo, halafu vyoo na miondombinu mingine”. Aliongeza mwaluka. 
Meneja
 huyo alisitiza kuwa wapenda michezo jijini Mbeya ambao ni mashabiki wa 
timu za Mbeya  City na Tanzania Prisons wasiwe na wasiwasi kwani timu 
zao zitatumia uwanja huo, na kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa 
ligi kuu januari 25, uwanja utakuwa bora”. Alisema Mwaluka.
Endapo
 uwanja huo hautarekebishwa kwa haraka, timu mbili za ligi kuu Mbeya 
City na Tanzania Prisons zipo hatarini kucheza nje ya Mbeya, kitendo 
ambacho kitawanyima fursa kuzishangilia timu zao kwa wingi.


No comments:
Post a Comment