ZAIDI ya wanafunzi pamoja na
vijana elfu kumi kutoka katika wilaya za Arusha na Meru wanatarajia
kunufaika na mradi wa afyaa ya akili ambao unalenga kuwafanya vijana kuepukana na madhara mbalimbali yanayowatokea
Hata hivyo mradi huo unatekelezwa
chini ya shirika la Farm Radio kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
ambao wote kwa pamoja wana malengo ya kuwakomboa vijana
Akiongea kwenye uzinduzi wa
kampeni shirikishi mapema jana mratibu wa mradi huo kutoka katika
Shirika la farm radio, goodlove Nderingo alisema kuwa mradi umeanza
rasmi toka mwezi September
Nderingo alisema kuwa mpaka sasa
utawasaidia vijana kutoka katika vituo lakini pia hata wanafunzi kutoka
katika shule 35 za Arusha vijijini lakini pia hata katika wilaya ya Meru
Alidai kuwa kutokana na jamii
kushindwa kujua umuhimu wa afya ya akili hasa kwa vijana kumesababisha
vijana wengi kushindwa kufikia malengo yao huku kundi kubwa nalo likiwa
linaendelea kuteseka kwenye jamii
Alisema, wamedhamiria kutoa elimu
ambayo itaweza kuwasaidia makundi yoye kwenye jamii wakiwemo wazazi
lakini pia hata walezi na walimu ambao wakati mwingine wanakuwa mwiba
kwa vijana hususani wale wenye matatizo ya akili.
“takwimu zinaonesha kuwa asilimia
kubwa sana ya vijana wameathirika na matatizo haya ya afya ya akili na
wanakosa msaada kwa kuwa baadhi yetu tulio wakubwa bado hatujaweza
kuelewa vyanzo vya haya yote lakini tutaweza kuwaelimisha hawa vijana na
wanafunzi ili wafike pale ambapo taifa limethamiria wafike’aliongeza
Nderingo
Naye mwakilishi wa walimu ambaye
ni Slyvester Paul aliongeza kuwa mpango huo wakuwelimisha jamii
kuhusiana na afya ya akili pamoja na walengwa wenyewe ambao ni vijana na
wanafunzi wa shule kutaweza kupunguza matatizo mbalimbali ambayo yamo
kwenye jamii
Paul alibainisha kuwa hata kwa
upande wa walimu nao wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanajijengea tabia ya
kuwasoma wanafunzi wao hasa wanapobadilika kwani wakati mwingine yapo
baadhi ya matatizo ambayo yanasababisha hata wanafunzi hao kubadilika
No comments:
Post a Comment