Naibu
Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,na
Mwenyekiti wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii
ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha, Mh. Aggrey
Mwanri, akiendesha shughuli za mkutano huo uliomalizika hivi karibuni
katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC).(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Mwandishi wetu, Arusha
MTAALAMU
mmoja wa masuala ya uchumi anayefanyakazi na Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo, ameishauri
serikali kutumia neema ya gesi kutoa hifadhi ya kutosha kwa wananchi
wake.
Dhliwayo
alisema hayo wakati akijibu hoja ya Naibu waziri Afya na Ustawi wa
jamii, Dk Kebwe S. Kebwe namna ya kufikia lengo la hifadhi ya jamii kwa
wote kwa kasi kuliko ilivyo sasa ambapo inafikiriwa ifikapo mwaka 2025
ndio tutakuwa tumefikia asilimia 75 ya hifadhi ya jamii.
Dk.
Kebwe alisema hayo wakati wa kujadili mada ya uchokozi iliyotolewa na
Dhliwayo mtaalamu wa uchumi ambaye alishawahi kufanyakazi nchini
Zimbabwe na Msumbiji.
Alisema kwamba mataifa mengi yametumia raslimali zao kufanya mambo makubwa kwa wananchi wao na Tanzania inaweza kufanya hivyo.
Ofisa
anayeshughulikia sera za hifadhi, UNICEF Tanzania, Bi. Usha Mishra
akitoa mrejesho walichojifunza washiriki siku ya kwanza na kutoa
mwongozo wa mambo mapya wanayotakiwa kujifunza katika mkutano
uliomalizika hivi karibuni jijini Arusha.
Alisema
ipo nchi ambayo ilitumia utajiri wake wa almasi kutengeneza miundombinu
ya barabara na si vibaya kwa Tanzania kutumia utajiri wake wa gesi
kuhakikisha kila mtanzania anapata hifadhi ya jamii.
Alisema
kama taifa linaweza kuamua asilimia Fulani kutoka katika sekta ya gesi
kuingia katika kuwezesha hifadhi ya jamii ambayo itahakikisha uwapo wa
huduma sawa kwa wote.
Alisema
uchumi wa Tanzania kutoka mwaka 2000 hadi sasa umekuwa ukikua kwa kasi
ingawa kasi hiyo haionekani kwa wananchi ambapo wengi wamejikuta wakiwa
katika umaskini wa kukithiri.
Alisema
kutokana na tatizo hilo la umaskini wa kukithiri kutoondoka kwa hali
hiyo kunasababisha na sekta husika kutotoa ajira za kutosha ambazo
zingewezesha watu kuneemeka na uchumi unaokua kwa kasi.
Mtaalamu
wa masuala ya uchumi anayefanyakazi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo akitoa mada chokonozi
wakati wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa
na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha ambao umemalizika hivi
karibuni jijini Arusha.
Alisema
aidha kaya nyingi zimekuwa na idadi kubwa ya watu ikiakisi umaskini
unaoambatana na kaya zenye watu wengi na uzazi wa mapema unaowakuta
wasichana.
Alisema
pamoja na mpango mzuri wa serikali kupitia TASAF kupunguza umaskini wa
kukithiri ukishirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa, ipo haja kwa
serikali kuhakikisha kwamba kunakuwa na uratibu unawezesha mipango ya
kupunguza umaskini inafanikiwa.
Alisema
iwapo TASAF inashughulikia elimu na afya ni dhahiri itahitaji kuwapo
kwa shule na walimu na katika afya hospitali na wauguzi na madaktari na
dawa.” Ni lazima kuwepo na uratibu ili kufanikisha yote yaliyolengwa”
alisema Dhliwayo.
Alisema
Tanzania inaweza kujifunza kutoka mataifa ya Rwanda na Eritrea ambayo
yamefanikiwa hifadhi ya jamii eneo la afya kufikia zaidi ya asilimia 90
huku wakitumia mifumo thabiti ya afya ya jamii kwa kaya.
Aidha amesema kwamba mataifa hayo yamefanikiwa katika malengo ya millennia na kupunguza idadi ya vifo vya wanawake katika uzazi.
Katika
mkutano huo ambao uliitishwa na serikali ili kupata misingi ya
utengenezaji wa sera na sheria ili kuwezesha watanzania wote kuwa na
haki katika kei ya taifa kw akuwezeshwa kuondokana na umaskini wa
kukithiri ulihudhuriwa na watalaamu 150 kutoka nchi mbalimbali duniani.
Pia
ulifunguliwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi
ambaye alisema Tanzania kwa sasa inapojianda kuwa na uchumi wa kipato
cha kati ipo haja ya kuimarisha sekta za hifadhi ya jamii.
Mkurugenzi mshiriki anayeshughulikia masuala ya program kutoka makao makuu ya UNICEF, Bi. Alexander Yuster akichangia hoja wakati wa mkutano huo uliomalizika hivi karibuni.
Meneja
Mwendeshaji wa Shirika la Under The Same Sun, Gamariel Mboya akiuliza
swali kuhusiana na serikali imejipangaje katika kuhakikisha watu wenye
ulemavu wa ngozi wanapataje mafuta ya kuzuia mionzi ya jua inayopelekea
ugonjwa kansa ya ngozi.
Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe Kebwe, akijibu swali
kuhusiana na serikali imefanya nini kwa walemavu wa ngozi katika
kuhakikisha mafuta kuzuia mionzi ya jua kwa watu hao yanapatikana
kiurahisi ili kupunguza athari za kansa kwa walemavu hao. Kulia ni Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.
Mwakilishi
wa wazee waliostaafu akiuliza swali kwa Wizara ya afya na ustawi wa
jamii kuhusiana na uboreshwaji wa huduma za afya kwa wazee ambapo
imekuwa changamoto kubwa kwao.
Mtaalamu wa mawasiliano wa Shirika la UNICEF Tanzania, Jacqueline Namfua akifurahi jambo wakati wa mkutano huo.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, watengeneza
sera, watafiti na waendeshaji wa mifuko ya hifadhi kutoka mataifa ya
Kenya, Uganda, Bangladesh, Mozambique, Lesotho, Malawi, Afrika Kusini,
Ghana, Ethiopia, Zambia, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania uliomalizika
hivi karibuni jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment