Kampuni
ya Twiga Cement ya jijini Dar es Salaam, jana imefanikiwa kuzindua
rasmi Chama cha Wachezaji wa Nafasi ya Golikipa wanaoshiriki ligi kuu ya
Vodacom Tanzania, ambapo katika uzinduzi huo timu hiyo ya Makipa
ilicheza mchezo wa Kirafiki dhidi ya Timu ya Kombaini ya Waandishi wa
Habari TASWA F.C.uliofanyika kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama jijini
Dar es Salaam jana.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa na
Ushindani wa Kipekee kutokana na Timu zote kuwa na Wachezaji Nyota na
Tegemeo katika Vipaji vyao, Mashabiki waliofika kushuhudia mchezo huo
walifurahishwa na jinsi kila mchezaji alivyoonyesha Ujuzi binafsi na
kiwango cha hali ya juu.
Timu ya makipa ndiyo iliyokuwa ya kwanza kufanya shambulizi
kwenye lango la timu ya TASWA ambapo dakika ya 26 mchezaji Shaaban Kado
alikosa Penalt kutokana na beki wa Taswa Martin Peter kunawa akiwa eneo
la kumi na nane na penalt hiyo ilidakwa na kipa nyota wa TASWA Ahmed
Famau.
Hadi kipindi cha kwanza
kinamalizika kikosi cha timu ya Makipa kilikuwa mbele kwa bao
1-0,lililofungwa na Juma Kaseja baada ya kutokea piga nikupige langoni
mwa TASWA, ambapo kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko ambapo
Taswa iliwatoa, Majuto Omary, Ibrahim Masoud, Ally Mkongwe, Zahoro
Mlanzi, Shafii Dauda, na nafasi zao kuchukuliwa na Salum Jaba, Juma
Ramadhani, Hatibu Naheka,na Paul Limoy,mabadiliko ambayo hata hivyo
yalishindwa kupunguza kasi ya wachezaji hao Makipa wa Ligi kuu waliokuwa
muda wote wakilisakama lango la TASWA FC.
Pamoja na kuwa na wachezaji wa
akiba timu ya Makipa lakini walishindwa kufanya mabadiliko, kutokana na
wachezaji wengi kuwa na pumzi ya kuwamudu TASWA ambapo Makipa hao
walisaidiwa na mlinda mlango kutoka timu ya Taifa ya Wanawake Twiga
Stars, Fatuma Omary ambaye hata hivyo alionyesha kiwango kikubwa baada
ya kudaka michomo ya wazi kutoka kwa washambuliaji wa Taswa,Ibrahim
Masoud, Shafii Dauda,Majuto Omary pamoja na Ally Mkongwe waliokuwa
wakilisakama Lango la timu ya makipa kila wakati.
goli la pili lilipatikana kunako
dakika ya 67 kupitia kwa Ivo Mapunda aliyefunga kwa shuti kali
lililomshinda mlinda wa TASWA Ahmed Famau,kabla ya shaaban Kado
kuhitimisha Kapu la Magoli kwa timu hiyo ya Makipa.
Pamoja na Kufungwa kwa Taabu 3-0
timu ya TASWA FC, iliweza kuwachezesha mputa mputa wachezaji hao nyota
wa Ligi kuu pamoja na kwamba wachezaji hao muda mwingi wanakuwa kwenye
Mazoezi Makali na Timu zao za ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara,kitendo
ambacho kiliwafanya kuonekana wakiwa na Uhai wa kukimbiza huku na kule
katika kipindi cha dakika zote za mchezo.
Taswa ambayo kwa asilimia kubwa
iliwachezesha wachezaji wake wengi ambao ni wafanyakazi wa vyombo mbali
mbali vya habari, ilisifiwa na mashabiki waliohudhulia mchezo huo kwa
kuwa Muda mwingi wanakuwa katika shuguli za kiofisi ambapo kwa mujibu wa
Mwenyekiti wa Timu hiyo wachezaji ukutana mara moja kwa wiki kwa ajili
ya mazoezi ya Pamoja.
“timu yetu ni nzuri sana hii
TASWA, mwenyewe umeona wachezaji walivyowapeleka mpuata hawa Makipa
pamoja na kwamba hii timu ya Makipa ni Wachezaji wa ligi kuu, nasema
ligi kuu kwa kuwa wanashiriki hiyo ligi isipokuwa tofauti wao ni makipa,
na tunapozungumzia suala la Wachezaji, mwenyewe unajua timu ili iwe
bora ni lazima kwanza iwe na Makipa wazuri ndipo iwe bora, na kipa bora
ni yule anayeweza kuwapanga wachezaji wake, hivyo kama hawa wachezaji
ndiyo wapangaji wa timu zao wakati wa Mashindano, mimi nasema tumecheza
na Timu ya Taifa na si kama unavyofikili wewe, na ndiyo maana nathubutu
kusema kuwa kufungwa kwetu mabao 3-0 ni sawa na kupata ushindi sisi,
maana hata hivyo wametuleta kwenye Uwanja wao, nadhani wakati wa mchezo
wa Marudiano bila shaka itakuwa zamu yetu kuibuka na ushindi maana leo
wameshinda wao na mpira ni mchezo wa mmoja kushinda, asiyekubali
kushindwa siyo mshindani” alisema majuto
na kuongeza kwamba mchezo huo kwa
pande zote mbili umewapa changamoto ya kuifanya sasa timu hiyo ya
Kombaini ya Makipa kutambuliwa kote Nchini.
“mkakati uliopo sasa ni kuhakikisha kwamba timu hii inazunguka
kwenye Majiji Makuu kwa ajili ya kufanya michezo yake ya kirafiki na
timu za Mikoa, lakini lengo kubwa ikiwa ni kuwapa Fursa wakazi wa Maeneo
hayo kuwatambua zaidi hawa Makipa wetu, lakini pia wakati wachezaji
hawa wakiwa kwenye hayo maeneo ya Majiji watakuwa na jukumu la kuwaandaa
wachezaji wengine zaidi vijana katika nafasi za kipa ili kuweza kuwa na
Makipa wengi zaidi kwa ajili ya Faida ya Taifa letu la Tanzania”
alisema Majuto
Naye kocha wa Taswa FC Ally
Mkongwe wakati akizungumza na wachezaji wa timu zote alisema kuwa ni
jambo la kufurahisha ambalo limeweza kufanikiwa kwa asilimia 100 kwa
kuwa lengo ilikuwa ni kufanya uzinduzi na timu zote zimeweza kucheza kwa
hali kubwa bila vurugu wala kuonyeshana mchezo mbaya.
“tumefurahi sana, niwapongeze
wachezaji wote yaani Makipa na Taswa, jambo hili si la mzaha kama
tulivyofikili hapo mwanzo, lakini kumbe mwitikio wa watazamaji ulikuwa
ni mkubwa sana na wengi wamekuja kuwatazama wachezaji na Waandishi wa
habari, Watangazaji, na wakati umefika tukae tuangalie namna ya
kuboresha mahusiano haya yawe ya kudumu baina ya TASWA na timu hii ya
Kombaini ya Makipa wa Ligi kuu, isipokuwa tusameheane kwa yale Mapungufu
madogo yaliyotokea maana sisi ni binadamu lakini wakati mwingine
nadhani hayatatokea kwa pande zote mbili endapo yametokea kwa mchezo wa
leo” alisema Mkongwe.
Hata hivyo wachezaji hao Makipa
wametakiwa kufanya jitihada za kuhakikisha wanakuwa chachu ya kuleta
Makipa wengine nyuma yao kutokana na kwamba nafasi ya Makipa kwa
Tanzania inazidi kupungua kutokana na nafasi hiyo kuwa ngumu
ukilinganisha na nafasi za wachezaji wengine wa ndani ambao wanakuwa ni
wengi.
Naye mmoja wa Makocha wasaidizi wa
timu ya TASWA Ibrahim Masoud aliwaasa wachezaji hao kuwa kioo kwa
wenzao na kuwa kishawishi cha kuwapata vijana wengine watakaokuwa makipa
wa Tanzania miaka ijayo”Sina Mengi ya Kusema kwa kuwa Kocha na
Mwenyekiti wameeleza kwa kirefu lakini mimi niko tofauti kidogo na
wenzangu, kikubwa hapa mimi ni kuhusu nyie Makipa wetu, kumbukeni kwamba
nyinyi kina Kaseja, Ivo Mapunda, Shaaban Kado, Dida, mstafa na nyinyi
wote, nyie sasa mnaelekea Ukingoni, ni kama kina Mwameja wakati wao,
kina Manyika, Mfaume,nk, walikuwapo lakini walipopotea hao makipa
Tanzania iliyumba sana kuwapata nyinyi, na hiyo inatokana na kwamba
Wachezaji wengi Makipa hawapati Fursa ya kuandaliwa, na niwatake sasa
kutumia mwanya huu kwa kuwa tayari mmekuwa ni makipa Hodari kuhakikisha
kwamba wakati wa Mapumziko ya Ligi, muweze kuingia Darasani kwa ajili ya
kupata ujuzi wa kuwa Walimu wa Makipa, Kila mmoja kwa wakati wake lengo
mtakapomaliza muda wenu wa kuitumia Tanzania katika Soka, muweze kuwa
walimu wazuri na wazalishaji wazuri wa Makipa wengine” alisema Ibrahim
Masoud(Maestro)
Kwa Upande wao Makipa hao wao
hawakuwa na la kusema isipokuwa kwa niaba ya wachezaji wote wa Makipa
Ivo Mapunda alisema kuwa wanashukuru kwa Sapoti kubwa kutoka Chama cha
TASWA, ambao mara zote wamekuwa mstari wa mbele kuwapa maelekezo,
kitendo kilichowaweka karibu zaidi hata wakati wa Uzinduzi wa Chama
hicho cha Magolikipa,” Sisi binafsi tumefurahi kukutana na timu hii ya
TASWA, maana kiujumla wachezaji wengi wa Taswa wanafahamu mpira, ila
tumewafunga kutokana na kukosa Pumzi tofauti na sisi wengi tunafanya
mazoezi kila siku na timu zetu tena timu kubwa za ligi kuu, mimi Kesho(
Leo) naelekea Zazibar Kambini, kujiunga na Timu yangu, kwa hiyo unaona
jinsi mchezo huu ulivyokuwa ni muhimu sana kwetu hata nimeshindwa
kuongozana na wachezaji wazangu pamoja na Mwalimu wangu kutaka nisicheze
hii leo lakini nimemkatalia kwamba ni lazima nijumuike na Makipa
wenzangu kwenye jambo hili la Umoja, maana sasa sisi Makipa pia tumekuwa
ndugu wa karibu na Marafiki wa Kweli, zama za kale kwamba huyu na huyu
aziivi eti kwa kuwa wote ni Makipa imepitwa na wakati, utatukuta mimi,
Kaseja, Kado, Dida, Mstafa, na wengine tukizungumza na kufurahi pamoja,
sisi siyo maaduni ni marafiki tena niwapongeze Wadhamini wa Mpambano
huu(Uzinduzi) Kampuni ya TWIGA CEMENT kwa kufanya jambo hili, limezidi
kutuweka karibu zaidi, na naamini kwamba watazidi kutuunganisha na
kuandaa michezo Mingi zaidi kwa ajili ya kuwapa Raha wakazi na mashabiki
wetu Mikoani” alisema Ivo Mapunda
Akizungumzia mchezo huo Afisa Masoko wa TWIGA CEMENT,Alex
Gideon, alisema kuwa maandalizi yamekwenda kama walivyopanga isipokuwa
mkanganyiko umetokea kwenye eneo dogo la Uwanja, ambapo awali mchezo huo
ilikuwa ufanyike kwenye uwanja wa KARUME kwa mujibu wa Matangazo
yaliyofanywa na vyombo vya habari,
” sitaki kulizungumzia sana suala la mkanganyiko wa Uwanja,
lakini nadhani TFF katika hatua za mwisho imeshindwa kuruhusu mchezo
wetu kufanyika kwenye viwanja vyao ambako vyombo mbali mbali
vilitangaza, hivyo mashabiki wengi walifika Karume, na nichukue fulsa
hii kuwataka radhi sana wote waliotufuata kwenye viwanja vya Karume,
mchezo wetu ulibadilishwa uwanja kutokana na sababu zilizokuwa nje ya
uwezo wetu na kwa kuwa ni TFF wenyewe waliopanga hatua za Mwisho Mchezo
wa Ligi daraja la kwanza kufanyika humo hatukuwa na kipingamizi, ni
jambo la kimchezo na ukizingatia ni ligi yetu pia sisi watanzania hivyo
hilo niombe radhi kwa mashabiki wetu wote, lakini kuhusu wadhamini wetu
kama ulivyoona mwenyewe wamejitaidi na huu ni mwanzo na maandalizi
yamefanyika kwa siku chache zana, wakati ujao tutaboresha na kulifanya
jambo hili kuwa la kudumu na lenye kuleta tija ya Maendeleo kwa hawa
Makipa wetu, kingine niwapongeze TASWA kwa ushirikiano wao maana
wametufariji na kutupa sapoti kubwa”
alisema Alex Gideon
aidha mchezo huo ulikuwa kwa ajili ya kujenga mahusiano mema
baina ya timu zote, wachezaji pamoja na kufanya Uzinduzi wa Chama cha
Makipa Tanzania, waandishi na Makipa wanaocheza ligi kuu Ya Vodacom
Tanzania.
No comments:
Post a Comment