Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd akikabidhi mchango
wake wa shilingi milioni 3 kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya Chuo cha
Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Mathew Luhanga (katikati) kusaidia
uboreshaji wa miundombinu ya chuo hicho jana usiku wakati wa harambee
maalum ya ukusanyaji wa fedha iliyofanyika Hotel ya Serena jijini Dar
es salamm.Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Prof. Emanuel Mjema.Picha na Aron
Msigwa – MAELEZO.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd na viongozi wa Chuo
cha CBE wakitoa mkono wa shukrani kwa wadau mbalimbali waliotoa michango
yao wakati wa harambee ya kuchangia maendeleo ya chuo cha CBE jana
usiku jijini Dar es salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 50
ya chuo hicho .
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd akisoma majumuisho ya
michango na ahadi zilizotolewa na wadau mbalimbali waliohudhuria
harambee ya kuchangia maendeleo ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jana
usiku jijini Dar es salaam. Kiasi cha shilingi milioni mia tano
arobaini, laki nane na elfu ishrini na tisa (540,829,000/=) zikiwa ni
ahadi na fedha taslimu zilikusanywa.
Baadhi
ya wadau wa maendeleo wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) wakitoa ahadi
na michango mbalimbali kusaidia maendeleo ya chuo hicho jana usiku
wakati wa chakula cha hisani cha miaka 50 ya CBE kilichoandaliwa na
uongozi wa chuo hicho kusaidia ukusanyaji wa fedha za ujenzi wa
miundombinu,vyumba vya mihadhara na madarasa vya chuo hicho.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd na viongozi wa Chuo
cha CBE wakitoa mkono wa shukrani kwa wadau mbalimbali waliotoa michango
yao wakati wa harambee ya kuchangia maendeleo ya chuo cha CBE jana
usiku jijini Dar es salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 50
ya chuo hicho .
No comments:
Post a Comment