Jaji Fredrick Wambali akitoa mada katika mkutano huo.
 Wanachama
 wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), wakiwa kwenye mkutano 
wao mkuu uliofanyika Dar es Salaam jana. Mkutano huo ulihudhuriwa na 
wanachama kutoka mikoa yote.
Wanachama
 wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), wakiwa kwenye mkutano 
wao mkuu uliofanyika Dar es Salaam jana. Mkutano huo ulihudhuriwa na 
wanachama kutoka mikoa yote.
……………………………………………………………………………………………
Dotto Mwaibale
JAJI Mkuu
 Mohamed Chande, amewataka wanawake nchini kutoa taarifa katika ngazi 
husika pindi  wanapoombwa rushwa ya ngono ili sheria ifuate mkondo wake.
Akizungumza
 wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa saba wa Chama cha Majaji Wanawake 
Tanzania (TAWJA), alisema kunaidadi kubwa ya wanawake ndani ya jamii 
wanaoombwa rushwa ya ngono lakini wamekuwa wahoga kutoa taarifa.
“Katika 
rushwa ya ngono lazima sheria mahususi zichukuliwe,hivyo tunawasihi 
wanawake baada ya kufanyiwa matukio hayo wafikishe malalamiko mahakamani
 au sehemu husika na sheria itafuatwa,” alisema Jaji Chande.
Kadhalika,
 serikali itaendelea kuboresha mazingira ya majaji wanawake ili 
kukabiliana na mabadiliko yanayoendelea ndani ya mahakama katika ngazi 
zote.
Mwenyekiti
 wa TAWJA, Engera Kileo, alifafanua katika kesi za rushwa ya ngono 
mahakama kupitia kifungu cha 25,muhusika atakayebainika kujihusisha na 
kitendo hicho atatozwa faini au adhabu ya kifungo cha miaka 30.
“Mahakama
 imeweka adhabu hiyo kutokana na ongezeko la matukio  kufanyika ndani ya
 jamii na wanawake kujengewa woga wa kutoa taarifa kwa wakati, hivyo 
tunachokifanya kuangalia namna ya kuongeza adhabu kwasababu ngono 
imetawala katika sekta mbalimbali,” alisema Kileo.
Lakini 
kwa sasa  chama hicho kinatoa elimu juu ya rushwa ya ngono katika jamii 
na matumizi mabaya ya ngono zembe ili kuwalinda na magonjwa ya 
kuambukizwa kama Maambukizi ya Ukimwi(VVu), na yale ya zinaa. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment