Meneja
 Tawala wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Gabriel Madembwe (katikati) 
akiwahutubia Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kutoka vitengo
 mbalimbali vya Makao Makuu ya Jeshi hilo wakati wa ufunguzi wa Mafunzo 
ya Takwimu Rasmi yaliyofanyika leo mkoani Morogoro. Kushoto ni Makamu 
Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Dkt. Frank Mkumbo na kulia
 ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza Makao Makuu Bw. 
Edward Kaluvya.
Baadhi
 ya Waandishi wa Habari wakichukua habari wakati wa ufunguzi wa Mafunzo 
ya Takwimu Rasmi kwa Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kutoka
 vitengo mbalimbali vya Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyofanyika leo 
katika ukumbi wa Amabilisi uliopo mkoani Morogoro.
Makamu
 Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Dkt. Frank Mkumbo akiwa 
katika mahojiano na Waandishi wa Habari mara baada ya ufunguzi wa 
Mafunzo ya Takwimu Rasmi kwa Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi la 
Magereza kutoka vitengo mbalimbali vya Makao Makuu ya Jeshi hilo 
yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Amabilisi uliopo mkoani Morogoro.
………………………………………………………………………………………..
Na Veronica Kazimoto
Morogoro
Wito umetolewa kwa Maafisa wa 
Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kutoka vitengo mbalimbali vya Makao 
Makuu ya Jeshi hilo kuwahimiza maofisa waliopo chini yao kutumia takwimu
 mbalimbali zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ili zisaidie 
katika kuandaa mipango na kutoa maamuzi mbalimbali ya kazi zinazofanywa 
na jeshi hilo.
Wito huo umetolewa leo na Meneja 
Tawala wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Gabriel Madembwe wakati 
akifungua Mafunzo ya Takwimu Rasmi kwa Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi 
hilo yaliyofanyika katika ukumbi wa Amabilisi uliopo mkoani Morogoro.
Madembwe amesema kuwa maafisa 
wengi katika Jeshi la Magereza wakijua umuhimu wa matumizi ya takwimu 
itasaidia kuleta mabadiliko hasa katika kupanga mipango yao kwenye 
maeneo yao ya kazi.
“Napenda kusisitiza kuwa ili 
mabadiliko yatokee sehemu yoyote ile; iwe nyumbani, kazini au katika 
jamii, ni lazima kuwepo na kichocheo cha mabadiliko hayo, hivyo ninyi 
mtakuwa kiungo muhimu katika kuleta mabadiliko yenye kutoa maamuzi kwa 
kuzingatia matumizi ya takwimu rasmi”, amesema Madembwe.
Nae Kamishna Msaidizi Mwandamizi 
wa Jeshi la Magereza kutoka Makao Makuu Dar es Salaam Bw. Edward Kaluvya
 amesema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka ambapo kwa sasa wamekuwa 
wakitumia sana takwimu katika maeneo mengi ya kazi zao.
“Mafunzo haya yatatusaidia kujenga
 uelewa wa pamoja na kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali 
yanayohusiana na uzalishaji, uhifadhi na utumiaji wa takwimu kwa usahihi
 katika kutoa maamuzi na kupanga mipango endelevu katika Jeshi letu la 
Magereza”, amefafanua Kaluvya.
Mafunzo haya ya siku tatu 
yanatolewa na Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo jijini Dar
 es Salaam na yamefadhiliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kupia Mpango 
Kabambe wa Kitaifa wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu Tanzania (TSMP).
Lengo kuu la Mpango huu ni 
kuhakikisha Tanzania inakuwa na mfumo imara wa kitaifa wa kuratibu, 
kukusanya, kuhifadhi na kusambaza takwimu nchini.
No comments:
Post a Comment