Mkurugenzi
 Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini Bibi Upendo Sanga akifungu 
semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya 
Vijana iliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo 
jana katika Mkoa wa Mbeya. Waliokaa katikati ni Mwezeshaji kutoka Wizara
 ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa na kulia ni 
Afisa Vijana kutoka Wizara hiyo Bi. Amina Sanga.
Afisa
 Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina 
Sanga akiwaelimisha vijana wa Wilaya ya Mbeya Vijijini kuhusu mwongozo 
unaosimamia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wakati wa semina ya 
Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana 
iliyofanyika jana katika ukumbi wa Halmashauri hiyo Mkoa wa Mbeya.
Afisa
 Ushirika wa Wilaya ya Mbeya Vijijini Bw. Isaya Mwamarobo akifafanua 
jambo wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko 
wa Maendeleo ya Vijana iliyotolewa kwa vijana wa wilaya hiyo jana katika
 Mkoa wa Mbeya.
Vijana
 wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoa wa Mbeya walioudhuria 
semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya 
Vijana wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa semina hiyo.  
Afisa
 Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na 
Michezo Bi. Amina Sanga wapili kulia akizungumza na wanakikundi wa 
Wasamba Saccoss Wilaya ya Mbeya Vijijini walipowatembelea kukagua mradi 
wanaouendesha. Wakwanza kulia ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya 
Bw. Laurean Masele na watano kulia ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya 
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa.
……………………………………………………………………………………….
Na: Genofeva Matemu – Maelezo, Mbeya
Vijana wa Mkoa wa Mbeya Wilaya ya 
Mbeya Vijijini wametakiwa kutokuwa na tafsiri hasi kuhusu Mfuko wa 
Maendeleo ya Vijana kuwa ni takrima inayotolewa na serikali kwa vijana 
hivyo kuchezea fedha hizo na kushindwa kurejesha mkopo watakaouomba 
kupitia mfuko huo.
Hayo yamesemwa na Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, 
Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa wakati wa semina iliyotolewa kwa 
Vijana wa Mbeya Vijijini kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Stadi za 
Maisha, Ujuzi na Ujasiriamali jana Mkoani Mbeya.
 
Bibi Riwa amesema kuwa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana unahudumia 
vijana wote nchini bila kuangalia itikadi za kisiasa ukiwa na lengo la 
kuwakomboa vijana na kuinua vipaji vya vijana nchi nzima.
 
“Vijana ni taifa la leo na kesho likiwezeshwa taifa zima 
limewezeshwa, Wizara yenye dhamana na Vijana inalenga kuwafikia vijana 
wote nchini bila kuangalia itikadi za kisiasa kwani vijana wote ni wetu 
na tunatamani kuona vijana wanajiendeleza kufikia ndoto walizonazo” 
amesema Bibi Riwa.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbeya Vijijini Bibi Upendo 
Sanga amesema kuwa ni bahati ya pekee kutembelewa na ugeni kutoka Wizara
 ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivyo kuwaomba vijana wa Wilaya
 yake kuzingatia elimu watakayoipata na kusambaza elimu hiyo kwa vijana 
wengine wa Wilaya yake ambao hawakuweza kufika katika semina hiyo.
Bibi Sanga ameiomba Wizara yenye dhamana na Vijana kuendeleza 
programu ya kuwaelimisha vijana mara kwa mara na kuwahamasisha vijana 
kujiunga katika vikundi kwani ni raisi kusaidia vijana wakiwa katika 
vikundi kuliko kumsaidia kijana mmojammoja.
 
Akichangia wakati wa semina hiyo kijana Evans Bembeja kutoka 
Shirika la Efao linalojishughulisha na kilimo cha mbogamboga amesema 
kuwa vijana wengi hawaangalii mbele wamekua kwenye mwamko wa kisiasa 
wakiamini kuwa siasa ndio sehemu ya kupata pesa za haraka hivyo kuachana
 na fursa nyingine kama vile kilimo na ufugaji.
No comments:
Post a Comment