| Viongozi wa kanisa hilo wakimshangilia mbunge huyo kwa msaada wake | 
| Waumini wa kanisa hilo wakifurahia misaada ya mbunge wao | 
| katibu mwenyezi wa wilaya ya Ludewa Filix Haule (kushoto ) na mmoja kati ya madereva wa mbunge Filikunjombe Bw Andondile wakisogeza vinanda viwili vya kisasa kwa mbunge Filikunjombe | 
| Mbunge Filikunjombe kulia akikabidhi msaada wa vinanda kwa viongozi wa kwaya katika kanisa la RC Madunda | 
| Kiongozi wa kwaya kanisani hapo akifurahia msaada wa vinanda kulia na mbunge Filikunjombe | 
| Mbunge Deo Filikunjombe (kushoto) akikabidhi msaada wa kinanda kwa viongozi wa kwaya kwaya katika kaniksa hilo la RC Madunda leo | 
| Mzee Nkwera ambae ni mshauri wa kisiasa wa mbunge Filikunjombe akizungumza kanisani hapo | 
| Bw Mgaya akimshukuru mbunge Filikunjombe | 
MBUNGE wa   jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe  amechangia   kiasi cha Tsh milioni  15  kwa  ajili ya  ukarabati wa kanisa la Roman Katoriki parokia ya  Madunda  wilayani  Ludewa pamoja na  kusaidia   vinanda viwili kwa  kwaya  mbili kanisani hapo.
Akikabidhi msaada  huo   leo   mara  baada  ya  ibada  ya  jumapili  mbunge Filikunjombe alisema  kuwa amefika  kanisani  hapo baada ya kuomba kinada na  kwaya  ya  kanisa  hilo na  hivyo  kutokana na kuwepo kwa kwaya  mbili amelazimika   kutoa msaada  wa vinanda kwa kwaya  zote pamoja na  kusaidia kiasi hicho cha  fedha  kwa ajili ya  ukarabati  wa kanisa  hilo.
Kwani alisema  kuwa kanisa   hilo ni mmoja kati ya makanisa  makongwe yaliyojengwa  miaka  ya  1980 katika wilaya   hiyo ya  Ludewa na  kuwa kanisa   hilo ndilo kanisa la tatu kujengwa kwa  wilaya ya  Ludewa hivyo  linahitaji  kufanyiwa  ukarabati  mkubwa  ili  kuendelea   kuwafanya  waumini  wa kanisa   hilo  kupata  eneo la kuabudia.
Filikunjombe aliwataka    waamuni hao na  waumini  wa madhehebu mengine  katika wilaya ya  Ludewa  kuendelea  kumwombea afya njema  ili  kupata  nguvu ya  kuwaletea maendeleo kama  ambavyo  ameendelea  kufanya katika wilaya   hiyo  kama  njia  ya  kuwashukuru  wananchi  wake  kwa kumwamini katika  uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwa  kumchagua  kuwa mbunge  wa  jimbo hilo la  Ludewa .
“Imani ambayo  wenzangu  wananchi wa Ludewa  mlioionyesha  mwaka  2010 katika uchaguzi mkuu  kwa kunichagua kuwa mbunge kamwe  sitaacha kuwakumbuka   wananchi  wangu  wa Ludewa  kila ninapokuwa bungeni mawazo yangu  kurejesha  ahsante  yangu kwangu na  kuona   wilaya  yetu ya  Ludewa  inaendelea   kupiga  hatua”
Pia mbunge huyo  alisema  kwa  sasa  mkakati  wake na  wa  serikali ya Rais Dr  Jakaya  Kikwete  ni  kuona  ujenzi wa barabara  ya  lami
kutoka Njombe hadi Ludewa inajengwa na tayari wakandarasi wa
kuanza ujenzi huo wamekwisha patikana ndani ya miaka hii miwili bararabara hiyo itakuwa imejengwa na ujenzi wake utafanyika kwa awamu tofauti.
kutoka Njombe hadi Ludewa inajengwa na tayari wakandarasi wa
kuanza ujenzi huo wamekwisha patikana ndani ya miaka hii miwili bararabara hiyo itakuwa imejengwa na ujenzi wake utafanyika kwa awamu tofauti.
Hata hivyo  alisema  kuwa akiwa mbunge  wa  jimbo  hilo kamwe  hatakubali kuona   wana Ludewa   anawapelekea  maendeleo kwa upendeleo na  kuwa lazima  pande zote  ikiwemo la milimani  , mwambao wote  wananufaika na matonda  yake  kwa  kuwa na maendeleo  wote.
Kwa 
 upande  wake  katibu  wa itikadi  na uenezi  wa  mkoa  wa Njombe  
Honoratus Mgaya  akimpongeza  mbunge    huyo kwa  kuendelea   kusukuma  
mbele  maendeleo ya  jimbo  hilo ,alisema  kuwa kazi zinazofanywa  na 
mbunge  huyo  zimekipatia  heshima chama  cha mapinduzi (CCM) na  kuwa  
utendaji mzuri  wa kazi wa mbunge  huyo ndio ambao umeitangaza wilaya 
ya  Ludewa .
No comments:
Post a Comment